SIKU chache baada ya staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel
kuripotiwa kufunga ndoa mjini Dubai, mchumba wa staa huyo aliyetambulika
kwa jina moja tu la Jeff amesema kuwa, anashangazwa na Aunt kuolewa
huku akiwa na ujauzito wake, Amani linashuka na mistari ya habari hii.
Akizungumza na Amani jijini Dar hivi karibuni, Jeff amesema kuwa
taarifa za kuolewa kwa Aunt alizipata akiwa nchini China na kushtuka
sana.
“Kinachonishangza ni huyo jamaa anafungaje ndoa na mwanamke ambaye
ana ujauzito wangu wa miezi sita ambao aliondoka nao kwenda Dubai?”
alihoji Jeff.
Jeff aliendelea kutiririka kama mtu alikuwa akiimba mashairi ya
Muziki wa Injili kuwa, kingine kinachomuumiza ni tabia ya Aunt kumuomba
fedha za matumizi akiwa Dubai huku akijua kwamba amefunga ndoa na mtu
mwingine.
“Wanawake ni mama zetu lakini ni wauaji wakubwa, inakuwaje anagawa
mimba ya mtu kwa mwanaume mwingine halafu mbaya zaidi nilipokuwa China
kila wiki alikuwa akiniomba fedha za matumizi nami nikawa namuagiza
aende sehemu kuchukua kumbe ni mke wa mtu!” alishangaa Jeff.
Juhudi za kumpata Aunt ili kuthibitisha madai hayo ya ujauzito
hazikuweza kufua dafu baada ya simu yake anayoitumia huko Umangani
kutokuwa hewani.
Jambo lingine lililomshtua Jeff ni kusikia kuwa aliyemuoa Aunt huko
Dubai anaitwa Sunday Dimonte kwani msanii huyo ‘alisevu’ namba yake kwa
kutumia jina hilo.
“Nilipomuuliza kwa nini ananisevu kwa jina la Dimonte, Aunt
aliniambia kuwa jina hilo lilimaanisha mpenzi kwa Lugha ya Kifaransa,”
alisema kwa masikitiko Jeff.
No comments:
Post a Comment