Venus hana lake Wimbledon
Bingwa mara tano katika
mashindano ya tennis ya Wimbledon, Mmarekani Venus Williams, amesema
hana nia ya kustaafu, baada ya kuondolewa katika siku ya kwanza ya
mashindano ya mwaka 2012 ya Wimbledon, katika raundi ya kwanza,
aliposhindwa na mchezaji kutoka Urusi, Elena Vesnina.
Venus, mwenye umri wa miaka 32, na anayeugua ugonjwa unaofahamika kama Sjogren's Syndrome, alishindwa 6-1 6-3 siku ya Jumatatu.
Mpinzani wake Vesnina amepangwa katika nafasi ya 79 katika orodha ya wachezaji bora zaidi wa tennis wa kike ulimwenguni.
"Haiwezekani nipumzike tu na kukata tamaa," alielezea Williams.
"Sina muda wa kujisikitikia. Hilo sio jambo zuri. Nitautumia muda wangu katika mawazo yanayonipa nguvu. Ninaupenda mchezo huu."
Mara ya kwanza Williams kushindwa katika raundi
ya kwanza ilitokea mwaka 1997, wakati alipoingia pambano lake la kwanza
la Wimbledon, na wakati huo alikuwa hata hayumo miongoni mwa wale
waliopangwa katika mashindano hayo kama wachezaji bora.
Ni wanawake wawili tu ulimwenguni ambao
wameshawahi kupata ubingwa wa Wimbledon mara nyingi kumshinda Williams,
lakini tangu mwaka 2008, hajawahi kuibuka bingwa wa mashindano hayo.
Mara tu baada ya ushindi wake wa mwisho, iligunduliwa kwamba anaugua ugonjwa wa Sjogren's Syndrome, na ambao humfanya mgonjwa kujihisi ni mchovu mno, na katika sehemu mifupa inaungana, maumivu.
No comments:
Post a Comment