TIKETI ZA OLYMPIC ZAUZWA KIMAGENDO
Kamati kuu ya Olimpiki
inachunguza tuhuma kwamba baadhi ya wawakilishi wa Olimpiki wako tayari
kuuza maelfu ya tikiti ya michezo ya London, kwa magendo.
Kamati ya Olimpiki, IOC, imesema inazipa uzito tuhuma hizo zilizotolewa kwenye gazeti moja la Uingereza, Sunday Times.
Gazeti hilo limesema maafisa na mawakala, kutoka
nchi zaidi ya 50, walikuwa tayari kuwauzia tikiti waandishi wa habari
waliojifanya kuwa wanawakilisha walanguzi.
Tikiti za michezo maarufu zilipatikana kimagendo kwa bei mara kumi zaidi ya bei rasmi.
Waandalizi wa michezo hiyo mjini London
walisema, kuwa hakuna tikiti yoyote iliyonunuliwa kimagendo na waandishi
hao wa habari, ambayo imetokana na wao.
No comments:
Post a Comment