Rais mpya wa Misri atajulikana Jumapili
Tume ya uchaguzi ya Misri
inasema kuwa itatangaza Jumapili matokeo ya uchaguzi wa duru ya pili ya
uchaguzi wa rais uliofanywa mwisho wa juma lilopita.
Kila mmoja kati ya wagombea hao wawili amedai kuwa ameshinda, na kwamba ataunda serikali ya kuleta umoja nchini.
Wafuasi wa Muslim Brotherhood wamekuwa wakiandamana katika medani ya Tahrir kati ya mji wa Cairo, kudai matokeo yatangazwe.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema kila upande unaogopa kutatokea maafa endapo upande wa pili atashinda.