Musri wa Muslim Brotherhood mshindi
Mohammed Mursi ametangazwa mshindi katika uchaguzi wa Rais nchini Misri.
Mursi ameshinda kura kwa asili mia 51.7%
akimshinda mpinzani wake wa karibu Ahmed Shafik kwa mujibu wa tangazo la
tume ya uchaguzi wa juu wa Rais.
Mkuu
wa jopo la Majaji, Farouq Sultan, amesema kua wamezingatia malalamiko
466 kutoka kwa wagombea, ingawa matokeo ya uchaguzi hayatobalika.
Tangazo hilo lilifuatiwa na shangwe na
vigelegele katikakati ya medani ya Tahrir mjini Cairo ambako wafuasi
wengi wa Bw.Mursi walikua wamekuanyika.
Wafuasi hao wamekaa kwenye medani hio kwa siku
kadhaa wakionyesha msimamo wao wa kuchukia sheria kadhaa zilizotangazwa
na Baraza la juu la utawala wa majeshi ambayo wanadai zimeundwa ili
kupunguza mamlaka ya Rais na kuelekeza uwezo mkubwa kwa majeshi.
Wafuasi wa Bw.Shafiq nao waliweka kambi yao
katika eneo la kaskazini mwa mji ambako kuna makao makuu ya Tume ya
uchaguzi huko Nasser City.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi Jaji Sultan
alianza kwa kunena kua tangazo la matokeo ya uchaguzi yalikua yamezongwa
na shinikizo pamoja na hali ya wasiwasi.
Tume ya uchaguzi ilizingatia sheria
ilipochunguza visanduku vya kupigia kura, na Jaji.Sultan alisema hakuna
kilicho juu ya sheria.
Jaji huyo akaongezea kukanusha madai mawili
nyeti kuhusu njama za kuibia uchaguzi, kwamba baadhi ya karatasi za
kupigia kura ziliwekwa ndani ya visanduku tayari zikiwa na majina ya
mgombea wanayemtaka ashinde.
Hatimaye Jaji Sultan akamtangaza mshindi kua ni
Bw.Mursi ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Muslim Brotherhood cha
Freedom and Justice, Bw.Mursi.
Baada ya dakika kadhaa akitangaza marekebisho
kuhusu matokeo madomadogo ya kura ndipo akamtangaza Bw.Mursi kua mshindi
kwa kuzoa kura 13,230,131, na Bw.Shafiq akiweza kuzoa 12,347,380, sawa
na asili mia 48.27%.