BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Wednesday, June 27, 2012

KAMANDA KOVA AZUNGUMZIA KUTEKWA KWA KIONGOZI WA MIGOMO YA MADAKTARI, DK. STEVEN ULIMBOKA...!!!

 Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu tukio la utekaji  na kujeruhi lililompata kiongozi migomo ya Madaktari,Dk. Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinywaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam hapo jana.Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kutokana na swala la kiusalama na kutoharibu upelelezi,kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi. Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutokea nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo watachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo 
Waandishi wa habari wakimsikilza kamanda Suleiman Kova katika kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es salaam leo mchana.(Picha na Full Shangwe Blog) 
Dk. Steven Ulimboka akiwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana baada ya kutekwa na kupigwa vibaya usiku wa kuamkia leo na kuokotwa huko Mabwepande.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...