JIHADHARINI NA UTAPELI HUU...!!!
Kutokana
na Kupenda Kuchunguza Mambo hususani ya msingi sana. Niliona Tangazo la
Kazi Kupitia moja ya Blogu za Hapa tanzania nilihisi lakini Sikupenda
Kuhukumu bila Kuwa na ushahidi na ufahamu wa kutosha kuhusu hilo Swala.
Hilo
tangazo lilikua ni La Kazi nikaomba baada ya hapo wakaniambia nitumie
CV, na kujibiwa kuwa baada ya Siku Mbili za Kazi nitajibiwa. Niliomba
hiyo nafasi wiki iliyopita na Jana Nikajibiwa na Huu hapa Chini Ndio
Ujumbe niliotumiwa na Hao Wahuni wa Mtandaoni ..
Habari,
Ninayofuraha
kukufahamisha kuwa ombi lako la kufanya kazi na Mercycorps
Nicaragua(Central America) limekubaliwa,nimeambatanisha barua ya
kukubaliwa ambayo utasaini panapohusika na kuirudisha kwetu.
Kwa
mujibu wa sheria za immigration hapa Nicaragua,NGO inatakiwa kukuombea
Visa/work permit ili uweze kuja hapa kuanza kazi,kwa sasa hakuna ubalozi
wa Nicaragua hapo Tanzania.
Kama
ambavyo nilikutaarifu hapo awali unatakiwa kutuma malipo kwa ajili ya
kuprocess Visa/Work permit yako mapema kama ambavyo barua ya kukubaliwa
kazi inavyojieleza ili kutoa muda mzuri kwa NGO kuprocess kwa wakati
ambapo itachukua siku 4 za kazi kupata kibali hicho cha Visa/Work
permit.
Sasa
katika kurahisisha utumaji wa malipo hayo Management imeomba kutumia
account ya mfanyakazi ambaye yeye ana account ambayo ni International
Account ambayo benki yake pia inapatikana hapo nchini Tanzania,hii ni
kwa sababu ya kurahisisha na kuondoa gharama za utumaji na ucheleweshaji
wa kupata malipo kwa wakati.
Kwa
hiyo unachotakiwa kufanya ni kubadili hiyo dola $197 kuwa Tanzania
shillings ambayo ni sawa na Tsh.315,200/- ,harafu utadeposit hiyo
Tsh.315,200/- kwenye account ifuatayo;
Tafadhali
nakuomba uscan na unitumie payslip/Deposit slip baada ya kufanya malipo
kwa Sababu Management itaihitaji kwa sababu za kiofisi,
Bank Name: Stanbic Bank
Account Name: Jacob E.E
Account Number: 0140518946701
Visa Card Number: 4313321007132065
Regards
Lilian Kisanga
Project Manager
Mercycorps
Nicaragua
Kutokana
na Ujumbe huo Niliingiwa na Wasiwasi Sana na kujiuliza vitu vifuatavyo:
Iweje Swala la Kulipa pesa ya Visa/Work Permit niliambiwa ni USD 197
iweje sasa Nilipe kwa Tsh? Halafu pili Iweje Nilipe kwenye Account ya
Mtu binafsi? Baada ya hapo Ikabidi nifuatilie kuhusu hii account
ikanibidi niwasiliane na Stanbic Bank kwaajili ya Ufafanuzi zaidi na
Ubalozi wa Marekani.Huu hapa Chini ni Ujumbe niliopokea Kutoka Benki ya
Stanbic Bank.....unasomeka hivi
"
Habari Josephat,
Unashauriwa kwamba kwa sasa usiweke hela yoyote kwenye hiyo akaunti ya Jacob E.E.
Salamu,
Patricia
"
Ndugu Zangu Huu Ni Utapeli Kwahiyo Msitume.
Josephat Lukaza
Josephat Lukaza
No comments:
Post a Comment