Monday, April 15, 2013

WANAJESHI WA CHAD WAANZA KUONDOKA MALI

Serikali ya Chad, moja ya nchi iliyochangia
idadi kubwa ya wanajeshi kushika doria
nchini Mali, imeanza kuwaondoa wanajeshi
wake kutoka nchini humo. Taarifa hii ni kwa
mujibu wa rais wa nchi hiyo Idriss Deby.
''Jeshi la Chad halina uzoefu wa kupigana
katika mazingira ya mashambulizi ya kuvizia
ambayo ndio yanafanyika nchini Mali,''
alisema rais Derby.
Wanajeshi watatu wa Chad, waliuawa katika
shambulizi la kujitoa mhanga siku ya Ijumaa.
Aidha wanajeshi kutoka Chad , Ufaransa na
nchi zengine za kiafrika,
wamefurushawapiganaji wa kiisilamu kutoka
miji iliyo Kaskazini mwa Mali.
Lakini makabiliano yangali yanaendelea
katika sehemu zengine za jangwa la Sahara.
Wanajeshi 2,000 wa Chad walikuwa na
jukumu kubwa sana katika vita hivi hasa kwa
sababu ya uzoefu wao kupigana vita vya
jangwani.
Takriban wanajeshi 30 wameuawa ikiwa idadi
kubwa kulinganishwa na wanajeshi kutoka
nchi nyingine yoyote.
Watatu kati yao waliuawa katika shambulizi
la kujitoa mhanga mjini Kidal siku ya Ijumaa.
Rais Deby aliambia vyombo vya habari vya
Ufaransa kuwa wanajeshi wake
wameshatekeleza wajibu wao.
Ufaransa pia imeanza kuondoa baadhi ya
wanajeshi wake 4,000 ikitaka kusalia na
wanajeshi 1,000 nchini humo mwishoni mwa
mwaka.
Ufaransa iliongoza kampeni ya kuwapeleka
wanajeshi nchini Mali mwezi Januari,
ikisema kuwa wapiganaji wa
al-Qaeda, walitishia kuvamia mji mkuu,
Bamako.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...