Sunday, April 14, 2013

TIMBWILI....

Tukio hilo lililokusanya umati lilijiri maeneo ya Mwenge, Dar mishale ya saa 10 usiku ambapo mwanaume huyo, mkazi wa Tegeta, alikiri kupokea kipigo almanusra apoteze uhai kutoka kwa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina Neema Samson, mkazi wa Buguruni.

Lazima unipe changu: Neema Samson akiwa amemkaba mteja wake baada ya kushindwa kumlipa chake.

Habari za uhakika ni kwamba Neema alidai kuwa mwanaume huyo ambaye ni mume wa mtu ana tabia ya kumtafuta yeye kwa ajili ya huduma ya mapenzi lakini akishakidhi matakwa yake huwa hataki kutoa fedha kama wanavyokubaliana.

Mpaka kieleweke: Bwana Joseph akionekana kuzidiwa ubavu na mwanadada Neema.

TUJIUNGE ENEO LA TUKIO Fichua Maovu ikiwa mzigoni kunasa matukio machafu katika jamii likiwemo lile sugu la usaliti kwa wanandoa, ilipofika eneo la tukio, ilisikika sauti ikitokea gizani ikiita, mwizi…mwizi…mwizi…

Starehe gharama: Joseph akizidi kupewa hali ngumu na Neema, pembeni wananchi wakianza kusogea eneo la tukio.

Timu ya Ijumaa Wikienda ilitii sauti hiyo na kuelekea kule ilikokuwa ikitokea ambapo Neema alikuwa amemkwida shingoni Joseph huku akilalamika kuwa anataka ujira wake.

Lolote na liwe: Neema akizidi kumkomalia mteja wake huyo ampe chake bila kujali watu waliokuwepo eneo hilo.

SEKESEKE LAFUNGA MTAA Kutokana na sekeseke hilo la kupigana, watu kibao walitoka nje ya nyumba zao na kushuhudia kilichotokea ambapo walipigwa na butwaa huku wakilalamika kuwa waliamshwa usingizini na watu waliokuwa kwenye starehe zao.

Msaada: Baada ya wananchi kuona bwana Joseph azidiwa, waliamua kuingilia kati kumnusuru.

WAAMKA NA BOKSA, NIGHTDRESS Huku wakiwa na boksa, night dress, vipensi na wengine mataulo, majirani wa eneo hilo walimshuhudia Neema akiwa amemkaba Joseph shingoni hadi akashindwa kupumua na kusababisha hekaheka mtaa mzima.

Nataka simu yangu: Baada ya songombingo hiyo, Joseph alidai kukwapuliwa simu yake aina ya Nokia na kimada huyo. Hapa akijaribu kuichukua.

“Kha! Mwanamke amemkaba mwanaume anataka kumuua kisa ni nini?” alihoji mmoja wa majirani hao. Neema alikuwa akimnyonga Joseph kwa kutumia fulana yake akilalama kuwa amezoea kupewa penzi kisha kuingia mitini bila kulipa.

Mimi nataka hela yangu tu: Kimada akilazimisha alipwe pesa yake shilingi 15,000/= ili ugomvi uishe.

“Namjua ni mume wa mtu, ni kweli nimefanya naye mapenzi na kama hamuamini niwaoneshe (huku akipandisha nguo na kubaki mtupu), nataka buku kumi na tano yangu la sivyo namtoa roho,” alisikika Neema akifoka kwa hasira.

Simu: Hii ndiyo simu aina ya Nokia aliyokuwa anaidai bwana Joseph.

Wakiwa eneo la tukio, mjumbe wa nyumba kumi alifika na kuwashuhudia wakigaragazana mchangani ambapo Joseph alidai kuwa Neema alimwibia simu yake aina ya Nokia.

MJUMBE ATEMA CHECHE Kwa upande wake, mjumbe wa nyumba kumi alijitahidi kwa uwezo wake wote kuwaamua lakini ilishindikana kwani Neema aliendelea kumkwida Joseph akidai ujira wake kwani tayari simu aliyokuwa ameisunda kwenye nyeti, alikuwa ameshanyang’anywa na wasamaria wema

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...