Tuesday, April 16, 2013

MECHI YA AZAM& SIMBA YAINGIZA MIL 66

Release No. 064 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Aprili 15, 2013

Wachezaji wa Simba SC wakiwasalimia wa Azam FC kabla ya mchezo wao jana.

MECHI YA AZAM, SIMBA YAINGIZA MIL 66/-Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Aprili 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000 kutokana na watazamaji 11,458. Viingilio katika mechi hiyo namba 155 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,849,326.14.

Yanga na JKT Oljoro wakiingia uwanjani wakati wa mchezo wao juzi, Jumamosi.

WATAZAMAJI 11,021 WAZISHUHUDIA YANGA, OLJORO Watazamaji 11,021 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Oljoro JKT iliyochezwa juzi (Aprili 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 63,170,000. Viingilio katika mechi hiyo namba 156 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,853,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,636,101.69. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,552,501.25, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,531,500.75, Kamati ya Ligi sh. 4,531,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,265,750.37 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,762,250.29.

Boniface Wambura Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...