Thursday, April 18, 2013

MAPENZI YA MASTAR

HESHIMA ya ndoa ni kuishi kwa upendo na uhai wake uwe wa hali ya juu. Ndoa idumu basi, kifo ndiyo kiwatenganishe kama vitabu vya dini vinavyotufundisha. Kukua kwa utandawazi kumeleta taswira mpya katika sura ya wapendanao. Sasa hivi Mtanzania anaweza kuolewa au kuoa raia wa nchi nyingine na kupitia hapo tunapata kujua mila na desturi za mataifa mbalimbali duniani.

Mtanzania anaweza kujua tabia za watu wengine kupitia ndoa mseto iliyofungwa, hivyo kama Mtanzania ataoa au kuolewa na mtu wa taifa lingine halafu ndoa yao ikasuasua kutoka na tabia ya mtu husika, hakika hiyo itakuwa ni aibu kwa mhusika na taifa lake kwa jumla.

Nyumbani ni nyumbani, kwa kulitambua hilo leo tuitazame heshima ambayo mastaa wetu walioolewa au kuoa nchi jirani wamejijengea na matukio ya aibu waliyofanya.

MWISHO MWAMPAMBA

Kwa upande wake yeye alikutana na Meryl Shikwambane aliyekuwa mshiriki katika shindano hilo akiiwakilisha nchi ya Namibia. Walianza mapenzi taratibu na kama utani, vyombo vya habari vikaripoti, mapenzi yakashamiri kiasi cha kufikia hatua ya kufunga ndoa mwaka 2011.

Watanzania walitamani kuona mafanikio makubwa juu ya ndoa hiyo ambayo ilipata matunda baada ya kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye baba yake (Mwisho) alimuita Monkey (Nyani). Baada ya ndoa hiyo, Mwisho hivi karibuni akiwa Bongo ameripotiwa kuanguka kwenye dhambi ya usaliti wa ndoa ambapo anatajwa katika skendo ya kutoka na staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’.

Baby Madaha alipohojiwa kutoka na Mwisho kwa ushahidi wa picha alisema hakuna cha ajabu kwa sababu walishawahi kuwa wapenzi awali hivyo wamerudiana (kwa hiyo kurudiana kumo hata kama mmoja ameshaoa?!)

Hiyo ni aibu yetu, Mtanzania anaonesha picha mbaya kwa wenzetu. Hata kama Meryl hayupo Bongo, anapoona au kusikia matukio kama hayo kwa mume wake, anapata picha kwamba Watanzania siyo wastaarabu na si waaminifu.

UWOYA NA NDIKUMANA

Ndoa ya mwigizaji wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya na msukuma kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ nayo ni aibu nyingine! Bibie Mtanzania ‘pyuwa’ akakutana na jamaa huyo raia wa Rwanda, wakapendana, mwaka 2009 wakafunga ndoa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar.

Ndoa yao imekuwa ikisuasua, zaidi chanzo kikitajwa ni bibie huyo mwenye mvuto wa hali ya juu. Ametajwa kuisaliti ndoa mara kadhaa, likiwemo tukio bichi la kunaswa na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ katika hoteli ambako mpaka sasa haijajulikana waliingia kufanya nini.

Kwa tukio hilo hakika picha mbaya kwa tasnia pamoja na taifa kwa jumla imejionesha. Uwoya ameshindwa kuitumikia ndoa yake kwa uadilifu kama alivyoapa mbele ya padri matokeo yake imekosa uhai na kuwa katika hali ya kifo. Aibu sana!

MFANO WA KUIGWA

Kama ni pongezi basi zinapaswa kuelekezwa kwa mshiriki mwingine wa Big Brother Africa 2009, Mtanzania Elizabeth Gupta ambaye ndani ya mjengo alianzisha uhusiano wa kimapenzi na mshindi wa shindano hilo kutoka Nigeria, Kelvin Chuwang. Baada ya uhusiano huo waliamua wafunge ndoa mwaka 2010, hadi leo ndoa yao haijatetereka na ikiwa imezaa matunda ya kumpata mtoto mmoja. Wawili hao maisha yanaendelea bila kuwa na kwaro zozote.

TAHADHARI

Kama raia wengine wa mataifa ya nje wataendelea kuoa au kuolewa na Wabongo halafu usaliti ukawa wazi, kuna uwezekano mkubwa wa Tanzania kutafsirika vibaya mbele ya jamii ya kimataifa inayojua nchi yetu ni ya upendo, amani na uadilifu.Tafakari, chukua hatua!

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...