Thursday, April 18, 2013

JAMANI WEMA....ADAIWA KUJITONGOZESHA TENA KWA DIAMOND

Aibu imemshuka, imemfika, imemwenea na imemtapakaa kila upande, Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu. Hivi leo, endapo utamkuta Wema akiwa ametulia kisha ukamtishia ukitumia sauti ya juu kuyataja majina ya Diamond na Penny, kuna uwezekano mkubwa mrembo huyo akavunja mguu kwa kukimbia ‘spidi’ kali.

Ikamshuka Wema; Jumatatu iliyopita, usiku mkubwa, inadaiwa kuwa mrembo huyo akiwa katika hali ya utulivu kabisa, akaamua liwalo na liwe, hawezi kulikosa penzi la mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’, wakati ni wake tangu na tangu.

Simu ikapigwa; inadaiwa kuwa Wema aliamini Diamond hapindui kwake, kwa hiyo alipiga simu kwa kujiamini. Kilichozungumzwa; baada ya simu kupokelewa, inadaiwa kwamba Wema aliomba Diamond afungue moyo ili penzi lao lirudi kama zamani.

Diamond kwa misifa; Diamond kwa kiasi fulani alipikwa kimuziki na Dully Sykes ‘Mister Misifa’ na meneja wake wa zamani anaitwa Papa Misifa, kwa hiyo naye ni zao la Misifa. Misifa kazini; Diamond aliposikia sauti ya Wema ikimbembeleza, ‘bichwa’ likamvimba, papo hapo, akaanza kumrekodi mrembo huyo.

Kilichosikika; sauti ya Diamond inasikika kwa juu, huku ile ya Wema ikitokelezea kwa mbali. Kimazungumzo ni kuwa M’bongo Fleva huyo, anaeleza kwamba hivi sasa yupo kwenye uhusiano ‘siriaz’ na mtangazaji, Penniel Mungilwa ‘Penny’, kwa hiyo hawezi kumwacha. Eti Diamond hataki ‘drama’; mwanamuziki huyo, anasikika akimjibu Wema kwamba hawezi kurudiana naye kwa sababu itaonekana wanafanya drama (maigizo). Diamond anafunguka: “Hapa hakuna drama wala nini, wala sikufanyii drama. I am in love with Penny (nipo kwenye penzi na Penny) na wewe unajua. Sipendi na sipendezewi kwa sababu mwisho wa siku yatakuja kutokea matatizo, sitaki.” Penny naye; mrembo huyo anayemmiliki Diamond kwa sasa, aliingilia mazungumzo kati ya M’bongo Fleva huyo na Wema, kisha anasikika akimpa vidonge vyake, mrembo huyo: “Wema unaweza kutuacha tulale?” Wema akasalimia; mrembo huyo ambaye juzijuzi alikata shilingi milioni 13 kumtolea faini msanii Kajala Masanja na kumwokoa na jela, hakutetereka kusikia sauti ya Penny kwenye simu, badala yake akamsalimia: “Uko poa?” Penny akaliendeleza: “Yeah, niko poa mamy wangu. Hivi kwa nini hutaki kitu kitakachokufanya uwe na amani? Sisi hatutaki matatizo na wewe.”

WEMA ANASEMAJE? Alipohojiwa na paparazi wetu kuhusiana na ishu hiyo, Wema alikataa katakata kwamba sauti inayosikika kwenye rekodi ya mazungumzo hayo siyo ya kwake, akaongeza kuwa alishaachana na Diamond siku nyingi zilizopita na kamwe hawezi kufanya kitu kama hicho. “Hao kama wananichokonoa wapate ‘kick’ wafanye kimpango wao na siyo kutumia jina langu, mimi ni staa mkubwa Tanzania na kila mtu ananijua, waniache na maisha yangu kwa sababu sipendi kuongeaongea. Hata hili kama usingeniuliza, nisingesema chochote,” alisema mrembo huyo.

DIAMOND JE? Diamond alipozungumza na ripota wetu, alisema kuwa sauti hiyo alimrekodi Wema kwa lengo la kumwonesha ni kiasi gani hivi sasa yupo kwenye uhusiano ‘siriaz’ na Penny.

1 comment:

 1. Greetings, I believe your site might be having web browser compatibility issues.
  When I take a look at your blog in Safari, it looks fine however when opening in Internet Explorer,
  it has some overlapping issues. I just wanted to provide you with a quick heads up!
  Apart from that, wonderful blog!

  Check out my blog; Its About Time Grindstone Mattseh

  ReplyDelete

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...