Tuesday, February 5, 2013

MTOTO WA AJABU AZALIWA IRINGA

“HUJAFA hujaumbika, Mungu ana makusudi yake na yeye  ni muweza  wa  yote kwani ndiye  aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.” Hiyo ni kauli ya mzazi wa mtoto  Zawadi Godfrey Mwingune aliyezaliwa akiwa na macho matatu na kichwa mfano wa uyoga.
.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita mama mzazi  wa mtoto  Zawadi, Marthar Kitago (28) mzaliwa wa  Kijiji cha Kidegembye Lupembe wilayani Njombe mkoani Njombe  alisema  kuwa hadi sasa anamwachia Mungu ambaye ndiye amempa zawadi ya mtoto  huyo.
“Jumapili Januari 13, mwaka huu nilishikwa na uchungu nikakimbizwa katika  Kituo cha Afya cha  Kidegembye ambako sikukaa nikahamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Njombe  Kibena ambako nilifanyiwa upasuaji na kubahatika kumpata mtoto huyu.
“Niliogopa sana baada ya kuonyeshwa mtoto wangu
jinsi alivyo ila nilipiga moyo konde kwa kuwa ni damu yangu, tukampa jina la Zawadi, tukiwa na maana ni kutoka kwa Mungu,” alisema mama huyo wa watoto watatu.
Baba wa mtoto huyo, Godfrey Mwingune anayeendesha maisha yake kwa kilimo alisema kuwa hali ya afya ya mtoto huyo si nzuri kwani mbali ya kuzaliwa na kilo 4 na nusu, bado ana tatizo la uvimbe katika paji lake la uso unaofanana na umbo la uyoga pia  kichwani kuna kovu kubwa kama ncha mbili hivi ambalo linatoa usaha mwingi.
Akaongeza kuwa katika jicho lake la  kushoto kwa juu kuna jicho la pili na kufanya mtoto huyo kuwa na macho matatu ambapo madaktari  wamemshauri ampeleke katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Amesema fedha zinazotakiwa ili mwanaye apatiwe tiba ni shilingi 1,500,000 na amewashukuru wakazi wa Isimani ambao  wamemchangia shilingi 300,000 kwani yeye hana uwezo.

Walioguswa na habari hii wanaweza kumchangia mtoto huyu kupitia namba 0754 026 299 au   
0712 750 199- Mhariri.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...