Thursday, September 20, 2012

PADRI POLAND AWALISHA WANAFUNZI KRIMU ILIPAKWA KWENYE MAGOTI


Baadhi ya matukio ambayo wanafunzi wanalamba krimu iliyo kwenye magoti ya Pardi Kozrya.
POLISI nchini Poland wameanzisha uchunguzi dhidi ya Padri Marcin Kozyra wa Poland baada ya kupatikana kwa picha zinazowaonyesha wanafunzi wa kike na kiume wenye umri wa miaka 13 wakilamba krimu iliyopakwa kwenye magoti yake.
Kozyra pia ni mwalimu mkuu wa Salesian High School ambako inasemekana kitendo hicho  ni utamaduni wa ‘sherehe ya kuwapokea wanafunzi wapya’ kila mwaka.
Wanafunzi wakijiandaa kumlamba magoti padri huyo.
Picha hizo zinamwonyesha Kozyra akiwa amekaa kitini na akiwa amevaa kaptura na akiwa na fimbo.
Picha zingine zinawaonyesha wanafunzi hao wakitambaa katika ngazi za ghorofani katika mstari ambapo serikali ya Poland na watu wengine wamemelaani kitendo hicho.  Lakini pia baadhi ya wazazi wamemuunga mkono padre huyo wakidai pia kwamba inayoonekana kuwa ni krimu, ni dawa inayotumiwa wakati wa kunyoa ndevu.
Inasemekana padri huyo hatachukuliwa hatua yoyote lakini kitendo chake hicho kimelaaniwa.
                           Wanafunzi wakipanda ngazi kwa kutambaa kuelekea kwa Padri Kozyra.                                          

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...