Thursday, September 13, 2012

MZEE RWAKATARE, MAMA RWAKATARE WAZUA GUMZO


Mama Rwakatare (kulia) akiwa na Mzee Rwakatare.
Stori: Sifael Paul
HABARI ya mjini ni juu ya picha zilizosambaa mitandaoni zikimuonesha Mchungaji wa Kanisa la Assembles of God ‘Mikocheni B ‘Milima ya Moto’ la jijini Dar es Salaam, Dk. Getrude Pangalile Rwakatare zikimuonesha akiwa na mwanaume anayedaiwa ndiye Mzee Rwakatare ambaye ni mumewe hivyo kuibua gumzo kubwa.
Picha hizo zinazowaonesha wawili hao wakiwa kwenye meza moja wakifuatilia jambo, zilipigwa Mei 26, mwaka huu kwenye harusi ya mtoto wa mchungaji huyo aitwaye Mutta Rwakatare kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar.
Mtoto wa mchungaji Rwakatare aitwaye Mutta Rwakatare akiwa na mke wake siku ya ndoa yao.
Watu walioziona picha hizo mitandaoni na kuzitolea maoni walionesha kushtushwa baada ya kumuona Mama Rwakatare na mwanaume huyo kwani wengi walidai hawakuwahi kusikia kama mchungaji huyo ana mume.
Kwa upande mwingine wapo watu waliokwenda mbali zaidi na kudai kuwa walishatengana lakini kwa kuwa mtoto wao alikuwa akifunga ndoa ndiyo maana walikutana katika tukio hilo muhimu na la furaha.
“Sijawahi kumuona au kusikia habari za Mama Rwakatare na mwanaume lakini kinachoonekana labda waliachana zamani na hapo walikutana tu kwa kuwa mtoto wao alikuwa anaoa,” ilisomeka sehemu ya maoni hayo kwenye mtandao mmoja wa kijamii.
Kwa mujibu wa makabrasha ya Amani, mchungaji huyo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), amekuwa mstari wa mbele katika kutoa somo la ndoa kanisani kwake hivyo husifiwa kwa jambo hilo bila kujali kama ana mume au hana
.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...