Friday, September 21, 2012

Migodi Afrika Kusini ingali inatokota


Wachimba migodi Afrika Kusini
Wafanyakazi katika mgodi mmoja wa dhahabu nchini Afrika Kusini,AngloGold wameanza mgomo mpya ambao ni wa hivi karibuni kukumba sekta ya madini nchini humo.
Mgodi wa Kopanang anawaajiri wafanyakazi elfu tano na wanagoma wakitaka mishahara yao kuongezwa zaidi ya mara mbili hadi randi 12,500 au dola 1,513.
Mgomo huu unakuja siku moja baada ya wachimba migodi wa mgodi wa Marikana kusitisha mgomo wao baada ya kuafikia makubaliano kuhusu nyongeza ya mishahara.
Uchunguzi kuhusu vifo vya zaidi ya wachimba migodi 40 unatarajiwa kuanza tarehe moja mwezi ujao.
Waziri wa sheria, Jeff Radebe alisema kuwa familia za watu 34 waliouawa na polisi,watashauriwa kuhudhuria kwenye uchunguzi huo, na kwamba utachukua miezi minne kukamilika.
Afrika Kusini ni mojawapao ya nchi zinazozalisha madini kwa wingi sana duniani.
Zaidi ya asilimia themanini ya madini ya dunia ya Plattinum hutoka nchini humo.
Takriban wafanyakazi 15,000 wanaoajiriwa na kampuni ya dhahabu ya AngloGold wanagoma.
Inakisiwa asilimia saba ya uzalishaji wa dhahabu nchini Afrika Kusini uliathirika kutokana na migomo mingi ambayo imekumba nchi hiyo.
Mgomo huu wa hivi karibuni ulianza usiku wa kuamkia leo katika mgodi wa Kopanang Magharibi mwa mji wa Johannesburg.
Inaaminika kuwa mgodi huo huzalisha asilimia ishirini ya dhahabu inayotoka Afrika Kusini.
Matakwa ya wachimba migodi hawa ni sawa ya wale wa mgodi wa Marikana ambao baadaye walikubali nyongeza ndogo ya mishahara kuliko walivyokuwa wanadai.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...