Sunday, September 16, 2012

MCHUMBA WA OTILIA AKUTWA AKISALITIMCHUMBA wa Mnenguaji wa Bendi ya Extra Bongo, Otilia Boniface, Ally Mzae ‘Kinde’ amepondwa na baadhi ya watu wanaomfahamu baada ya kumbamba akidendeka na marafiki wa mchumba’ake.
Ishu hiyo ilijiri juzikati ndani ya Ukumbi wa Meeda, Sinza jijini Dar es Salaam wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza ambapo Kinde alinaswa kwenye pozi za kimahaba na Tingisha na baadaye kukutwa akiwa na Mwantum Athuman ambao wote ni wanenguaji wa bendi hiyo.
Paparazi wetu alimshuhudia Kinde akiwa bize kimahaba na Tingisha na baada ya muda alimdaka Mwantum na kuanza kupeana naye mahaba huku wambeya wakiwapiga chabo.
Baadhi ya wambeya hao walisema alichokuwa anakifanya jamaa huyo ni usaliti wakidai kama hana mpaka na shemeji zake, basi ni vyema angesubiri akiwepo Otilia mwenyewe.
Paparazi wetu aliongea na Kinde kuhusu ‘madudu’ aliyokuwa akiyafanya ambapo alisema mademu hao ni shemeji zake kwa hiyo haoni ubaya wa kujirusha nao hata kama Otilia hayupo.
“Hawa ni shemeji zangu, hata kama Otilia hayupo tatizo liko wapi? Mimi kwangu naona sawa tu,” alisema Kinde.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...