Thursday, September 20, 2012

KAMA ULIMIS UHONDO WA MECHI ZA LIGI KUU TZ, HUU HAPA YAKIWEMO MATOKEO YA MECHI ZOTE.


.
Ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara iliendelea tena september 19 ambapo timu zote 14 zimeshuka katika viwanja tofauti kutafuta pointi tatu muhimu ambapo Dar es salaam mabingwa watetezi wa ligi hiyo wekundu wa Msimbazi Simba wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa JKT Ruvu 2 kwa 0.
Simba imefanikiwa kupata ushindi huo ikiwa pungufu baada ya mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka Uganda Emmanuel Okwii kuonyeshwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza.
Magoli ya Simba yalifungwa na viungo Amri Kiemba na Haruna Moshi ‘Boban’ na kwa matokeo hayo, Simba inaendelea kuongoza ligi kwa kufikisha pointi sita baada ya awali kuifunga African Lyon 3-0.
Kocha wa JKT Ruvu Charles Kilinda amesema wamepoteza mchezo huo kutokana na kufanya makosa ambayo yamesababisha mabao mepesi kwa wapinzani wao lakini kocha wa Simba Milovan Cirkovic amesema haukuwa ushindi mwepesi hasa ukizingatia timu yake ilicheza pungufu kwa muda mrefu na amemlaumu mwamuzi wa mchezo huo kwa kusema kadi nyekundu aliyomuonyesha Emmanuel Okwii haikuwa sahihi kwani alistahili kadi ya njano.
Hiki ndio kikosi cha Mtibwa Sugar kilichocheza na Yanga.
Wakati Simba wakiwa Dar es salaam wapinzani wao Dar es salaam Young Africans walikuwa na kibarua kingine kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo Yanga walichapwa 3-0 hivyo Yanga waliziacha pointi tatu muhimu mbele ya Mtibwa.
Kwenye mechi iliyochezwa Mwanza Toto Afrika walilazimishwa sare nyingine katika uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 2 kwa 2 dhidi ya  Azam FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Tanzania Prisons na Coastal Union walitoka 1-1, Kagera Sugar na JKT Oljoro hawakufungana, kwenye game iliyochezwa Mbagala Chamazi African Lyon iliishinda Polisi Morogoro 1-0, Ruvu Shooting Stars wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani Pwani wameifunga JKT Mgambo 2 kwa 1.
Dar es salaam Young Africans kwa mara ya kwanza wataonekana jijini Dar es salaam katika ligi kuu ya msimu huu kwa kuvaana na JKT Ruvu kwenye uwanja wa taifa wakati Azam fc watajitupa kwenye uwanja wao wa Azam Complex Chamazi kuwakaribisha Mtibwa Sugar kutoka Morogoro.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...