Saturday, September 8, 2012

Jackline Wolper kuwania Ubunge 2015


Jackline Wolper


WAKATI baadhi ya wasanii wakishindwa kueleza wapo chama gani cha siasa, msanii anayechanua zaidi katika fani ya filamu bongo Jackline Wolper, inadaiwa kuwa anafanya mchakato wa kutaka kuchukua fomu kwenye moja ya vyama vyenye upinzani mkubwa Tanzania kwa ajili ya kungombea ubunge 2015 ingawa bado haijajulikana ni jimbo gani.

Wapo wasanii ambao waliwahi kuchukua fomu lakini baadaye walirudisha kwa madai kuwa fani zao za sanaa haziwezi kuendana na siasa, huku wakiamini kuwa watashindwa kupata mashabini kwani wanahisi wapo baadhi ya mashabiki wanaitikadi za kisiasa.

Rafiki wa karibu sana na msanii huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Irene, alidai kuwa msanii huyo yupo karibu na moja ya viongozi wa vyama viwili vya siasa vyenye ushindani mkubwa Tanzania lakini bado hajajua ataenda wapi.

Irene alidai kuwa uamuziki wa Wolper umekuja baada ya safari alizowahi kuzifanya bungeni na inaonekana shinikizo hilo limekuja baada ya kuonekana uwezo wake wa kujieleza na hata elimu yake vinaweza kumfanya akawa mwakilishi mzuri wa wananchi.

“Mimi siyo msemaji jamani pengine umuulize muhusika kwani nachoweza kukuambia ni kwamba anafanya mchakato wa kungombea ubunge na sijajua ni chama kipi kwani wapo baadhi ya wabunge ambao anazungumza nao kwa ajili ya ishu hiyo lakini bado hajawajibu lolote,” alisema Irene.

Mwandishi wa DarTalk hakusita kumtafuta mbunge huyo mtarajiwa ili afunguke kuhusiana na ishu hiyo na alipotikana mdada huyu alidai hakuna kisichowezekana chini ya jua na anaweza kuwa mbunge 2015.

Hata hivyo alishindwa kueleza uma kuwa atachukua nafasi hiyo kwenye chama gani au jimbo gani kwa madai kuwa bado mapema na mambo yatakapokuwa yameiva ataweka wazi.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...