Sunday, September 16, 2012

Irene Uwoya kufanya filamu ya kimataifa Uingereza


MSANII wa filamu bongo ambaye ni mama wa mtoto mmoja Irene Uwoya, ameondoka nchini hivi karibuni kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kampuni moja ya filamu iyomilikiwa na raia wa Nigeria na Ghana ili aweze kufanya nao kazi ambayo itakuwa ya viwango vya kimataifa.

Ingawa wapo wasanii wengi ambao wanaenda nchini humo kwa ajili ya matembezi tu lakini kwa upande wa uwoya nafasi hiyo ya kazi itakuwa ni njia moja ya kumtengenezea nafasi ya kufika kimataifa zaidi.

Uwoya akiongea na DarTalk kwa njia ya mtandao akiwa safarini alidai mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na hatua waliyofikia inaleta muafaka wa kufanya filamu. Awali kabisa msanii huyo aliwahi kuzungumza na mtandao huu na kusema kuwa anatarajia kufanya filamu na wasanii wa nchi mbili Nigeria na Ghana ambapo sasa anawathibitishia watanzania kuwa malengo yake yatatimia.

“Kwa sasa nipo Uingereza na kikubwa ambacho kimenileta huku nadhani niliwahi kukisema awali kuwa nahitaji kufanya filamu za kimataifa hivyo nipo huku kwa ajili ya mazungumzo na watu ambao wanahitaji kufanya kazi na mimi,” alisema.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...