Saturday, September 8, 2012

Herieth Amos Aongelea issue yake ya kuolewa na mtu mwenye umri kama baba yake

MSANII wa filamu bongo Herieth Amos, amefunguka kuwa kuolewa kwake mwanaume aliyemzidi umri na kuhongwa gari hakumaanishi kuwa amefuata hela pale ni mapenzi aliyonayo.

Msanii huyo anafanya vizuri kwenye tasnia ya filamu, na tayari ameshacheza filamu nyingi, ambazo zimemweka juu na kumtangaza katika tasnia hiyo.

Mwandishi wa mtandao wa DarTalk, baada ya kusikia maneno mitaani kuhusiana na ishu hiyo, alimtafuta msanii huyo na alipopatikana alidai kuwa anampenzi mume wake na haoni kama maneno ya watu yanaweza kumfanya asinywe maji au kufurahia mahusiano yao.

“Kuolewa na mtu mwenye umri mkubwa siyo tatizo kwani mapenzi hayana umri hivyo nachotaka kusema ni kwamba nampenda sana mume wangu na sijali juu ya maneno ya watu ambayo hayana msingi wowote,” alidai.

Hii ndio gari ya Harieth aliyonunuliwa na mumewe

Hata hivyo alioneza juu ya kuhongwa kwake gari baada ya kuolewa alidai kuwa hiyo ni zawadi kutoka kwa mume wake hivyo haoni sababu ya watu kuanza kuzungumzia vibaya ambapo pia anaamini kuwa watu wanaona wivu yeye kuolewa na baba huyo.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...