Thursday, September 13, 2012

HAYA NDIO MANENO MAPYA T.I.D ALIYOYAONGEA KWA DAKIKA MBILI KUHUSU ALLY KIBA, UGANGA NA HAWAMUWEZI..


.
Unakumbuka ni siku kadhaa zimepita toka kuandikwa kwa stori kubwa kwenye kiwanda cha bongofleva kuhusu T.I.D kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutaka kumuua msanii mwenzake ambae ni Ally Kiba?
Baada ya hiyo stori kutoka, kilipita kipindi kifupi cha ukimya lakini sasa hivi T.I.D ameongea kwa upana zaidi kuhuu hizo tuhuma ambazo zilimfanya ashikiliwe na polisi kwa mahojiano.
Kwenye 255 ya XXL Clouds Fm namnukuu akisema “hii kesi nashindwa kuielewa, mimi ni mtu mzima sana alafu ukiniambia nina matatizo na Ally Kiba na wakati hata sijagombana nae, hivi vitu hivi mtu unaenda kwa mganga unataka kujibust afu mganga anakwambia bwana T.I.D ujue katoa ngoma kali anataka kukuua we unachukulia serious, hivi vitu ni vya kijinga sana unatakiwa kufikiria”
Kwenye sentesi ya pili, T.I.D amesema “Polisi wamechukua pin namba yangu, sim namba yangu na kwenda kufanya uchunguzi hakuna connection yoyote ya mimi kwamba nimeongea na Ally Kiba au nimeongea na mtu yeyote ambae anataka kumuua Ally Kiba kwa hiyo ni uongo, sasa mimi kwa fikra yangu kama mtu mzima nafikiria huyu kijana huyu, mganga ambae amemshauri yeye ajibust kupitia section hiyo, amekoseaaa amekosea sana kwa sababu tunaamini kwenye kipaji”
Sentensi ya tatu ya maneno ya T.I.D ni “yeye kama anataka kuwa mkali kunizidi mimi ajifue atoe ngoma kali lakini hakuna mtu anaemchukia, mimi nampenda sana na kama yeye anakataa mimi simpendi kwa nini ameingia kwenye remix yangu na nimemuweka pale, remix nilitaka niitoe sema walivyoniweka ngome kidogo nimejisikia kama wananichukia, lakini mimi nitaitoa hii ngoma na mimi sijibust kama wanavyojibust na hawaniwezi”
Sentensi ya nne ya kauli ya Top in Dar ni “wanataka kuniweka ndani, wanataka kunifunga jela lakini mi naomba kabla hawajaniweka ndani niwape show hii apa ya usiku wa viuno sunday hapa kesho kutwa Bills, nitakua mimi na wakali wote Ngwea, Profesa Jay kwa sababu tunazindua ile single mpya ya ‘raha’ alafu kona lake”
Kuhusu kesi, namnukuu  T.I.D  akisema “kesi lazima iende kwa mwanasheria mkuu kuangalia kama inaweza kuwa kesi lakini imerudishwa imeonekana haiwezi kuwa kesi kwa sababu haina ushahidi wowote, inaonekana tu vitu vya imagination ambavyo mtu kapanga vifanyike lakini kwa sababu wao wanaendelea kutaka kesi na mimi nataka wao pia niwafungulie kesi kwa kunidhalilisha”

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...