BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Tuesday, September 4, 2012

Dogo Janja Ndani ya Beef Zito na Tunda Man na Maneck

Dogo Janja
 Maelezo ya Dogo Janja yanaamplfy kwamba juzi (September 2) walivyokua Club Maisha aliperform akiwa na furaha kutokana na mashabiki zake waliojitokeza na alipomaliza kuperform alishuka kwenye stage akiwa na furaha baada ya kufanya vizuri lakini hiyo furaha ilikatishwa baada ya kwenda juu sehemu ya V.I.P

Janja anasema alipopanda V.I.P kumsalimia Producer Maneck alimjibu kwa dharau na kumwambia haongei na Masnich hivyo Dogo Janja akaondoka lakini muda mfupi baadae alirudi na kukuta Tunda Man yuko karibu na alipokaa Maneck, Janja pamoja na Tunda walimsogelea producer huyo ambae alianza kumtukana matusi mazito Dogo Janja.

Baada ya hapo ilibidi Dogo Janja kushuka chini na kwenda kumchukua Ustaz Juma ambae ndio boss wa kundi alilopo sasa Dogo Janja la Watanashati, walipofika alipo Maneck.. alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja aliyorekodi na producer Marco Chali kwa kusema wimbo huo ambao mwanzo ulikua urekodiwe kwa Maneck ni wa kawaida sana.

Kwenye line nyingine namkariri Dogo Janja akisema “nikawa nimepanic sana sasa leo nakuja kupokea simu eti Tunda man nae anasema nifute chorus ya ‘Anajua’ kwenye wimbo wangu, Bro ule wimbo nimeurekodi nikiwa Tip Top na nimeifanyia show nyingi sana Tanzania ambazo zimewaingizia hela nyingi sana, hawana ubinadamu yani wanaponiambia mimi nifute chorus, Tunda kawafanyia watoto wangapi chorus? Shetta, Pasha lakini mbona hamwaambii Pasha afute au labda sababu mi mdogo, hili swala nawaachia watanzania kwa sababu ile ni haki yangu, nilimshirikisha Tunda.. ule wimbo sio wa Tunda siwezi kufuta chorus”

Baada ya hayo maelezo ya Dogo Janja, Producer Maneck amezungumza exclusive na millardayo.com na namkariri akisema “Dogo Janja alikuja akanisalimia nikamwambia ebwana eeeh kaa mbali na mimi sihitaji kuongea na wewe kwa sababu unatabia za kisnich sana, kuna vitu flani alivifanya siku kadhaa zimepita na sikupendezwa navyo.. tuliandaa show ya Tunda Man pale Maisha Club  tukamwambia na akakubali kufanya na tukatangaza kwamba atakuepo sasa mwisho wa siku akabroadcast msg kwenye BBM alafu sisi hakututumia ile msg ila akabroadcast kwa watu kwamba hao ni matapeli, hapohapo nachat nae namuuliza mbona umezingua anasema mi naona aibu sijui hata sura yangu sijui nitaiweka wapi kwa bwana Captain, huku anasema hivi huku anafanya hivi”

Tunda Man nae ametoa sababu za kumwambia Dogo Janja afute sauti yake kwenye kolabo waliyofanya ya ‘Anajua’ na nina mkariri akisema ” sikuzungumza kwa ubaya, nimezungumza kwa nia nzuri tu.. kwenye chorus inasema niko na Captain Tunda man alafu mimi siko pale mashabiki wanakua kama hawakuelewi vizuri, kuna mistari mingine inasema narun city nikiwa na JCB, narun Dar City nikiwa na T.I.P sasa ujue kwenye show kuimba vitu kama hivyo wakati hayupo na Tip Top vinakua havileti maana, ni kama maoni tu nimemuomba aimbie beat  kwa sababu anaweza kurekebisha ile mistari, mfano kusema narun city nikiwa na Watanashati, kwenye show ndio abadilishe lakini kwenye audio ni sawa ikibaki na vionjo vya mwanzo”

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...