Thursday, September 20, 2012

Diamond Aibiwa Vitu Jukwaani Abaki na Suruali na Boksa tualiyekuwa Dodoma ICON namba moja wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukombwa kila kitu na mashabiki wake na kubaki na suruali na boksa pekee. Tukio hilo lililoshuhudiwa na shuhuda wetu lilitokea kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma hivi karibuni ambapo kulikuwa na Tamasha la Serengeti Fiesta 2012. Akiwa stejini ‘akipafomu’ na zilipendwa wake Wema Isaac Sepetu, Diamond alikwenda kusimama kwenye ukingo wa steji sehemu ambayo ilikuwa na mashabiki wengi ambao walimvuta na kumdondosha chini kisha wakamsaula koti, tisheti, viatu, miwani, kofia na vitu vyote vilivyokuwa mifukoni na kumwachia suruali na boksa tu. Shukrani kwa mabausa ambao waliwahi kumuokoa kwani mashabiki hao walikuwa wakimvuta kila upande, hivyo kuwa na uwezekano wa kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...