Wednesday, September 26, 2012

Bond aaga dunia


John Bond
Meneja wa zamani wa Norwich na Man City
John Bond, aliyekuwa wakati mmoja meneja wa Norwich, na vile vile klabu ya soka ya Manchester City, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 79.
Katika kipindi cha miaka mitatu alipokuwa katika klabu hiyo ya Man City, Bond aliiwezesha timu hiyo kufika katika fainali ya Kombe la FA mwaka 1981, lakini walishindwa na Tottenham.
Vilevile aliiwezesha klabu ya Norwich kufika katika fainali ya Kombe la Ligi katika uwanja wa Wembley mwaka 1975, lakini Aston Villa ikaishinda timu hiyo goli 1-0.
Aliwahi kutoa mafunzo kwa vilabu vingi; Bournemouth, Norwich City, Manchester City, Burnley, Swansea City, Birmingham City, Shrewsbury Town na Witton Albion.
Kama mchezaji, aliichezea West Ham kwa muda wa miaka 16, na kucheza mechi 444, ikiwa ni pamoja na ushindi wa Kombe la FA mwaka 1964.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...