Friday, September 14, 2012

ALICHOSEMA ARSENE WENGER KUHUSU KUONGEZA MKATABA ARSENAL.


.
Kocha wa club ya Arsenal Arsene Wenger ambae ameifundisha club hiyo toka mwaka 1996 amekanusha kufanya mazungumzo yoyote ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuifundisha Arsenal.
Pamoja na kwamba Chief executive Ivan Gazidis aliweka wazi kwamba bado anamuona Wenger kama kocha anaefaa kuendelea kuwepo Arsenal, kocha huyo amesema bado ana miaka miwili iliyobaki kwenye mkataba wa sasa hivyo anatumia muda huo kujiangalia kama atafanya vizuri.
Wenger anatarajia kufikisha umri wa miaka 63 mwezi ujao ambapo Sky Sports wamemkariri akisema hafikirii kuwa kocha zaidi ya mwaka 2014, hata hivyo kwenye kauli nyingine aliamplfy kwamba kwa sasa anajiangalia tu kama hatofanya vizuri kama anavyotaka basi itabidi ajiondoe.
Mtu wangu wa Arsenal.. kuna umuhimu kweli Wenger kuendelea kuwa kocha wenu?

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...