BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Wednesday, August 1, 2012

ZIDANE KAWA KOCHA, HII NDIO TIMU ILIYOMPA KAZI.


.
Club ya Real Madrid imetangaza kwamba Mchezaji Legend wa soka wa Ufaransa Zinadine Zidane atakua kocha wa moja kati ya timu za vijana za Real Madrid.
Zidane mwenye umri wa miaka 40 ambae alistaafu kucheza soka miaka sita iliyopita baada ya kumpiga kichwa mchezaji Marco Materazzi kwenye fainali ya kombe la dunia ishu ambayo ilimfanya aape kwamba hatorudi tena uwanjani, anataka kurudi kwenye soka lakini akiwa kama kocha.
Mpaka sasa amezichezea club kama Cannes, Bordeaux, Real Madrid na Juventus ambako kote huko alifanikiwa kuzigonga nyavu mara 95 toka ameanza kucheza soka mwaka 1988.
Zinedine Zidane atakua anaendelea na masomo yake ya ukocha wakati akiifundisha timu hiyo ya vijana na anatarajia kumaliza hiyo kozi ya ukocha mwaka huu.
Zidane anatarajiwa kuchukua nafasi ya Alberto Giraldez kama mkuu wa timu za vijana wa Real ingawa club hiyo haijathibitisha hizo stori mpaka sasa.
Zidane ambae ameshinda mara tatu kuwa mchezaji wa dunia wa Fifa amewahi kusema kwamba ana ndoto za kuwa mwalimu wa soka siku moja na pia kuifundisha timu ya taifa ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...