Saturday, August 4, 2012

Uwoya, Tino waishi nyumba mojaINAWEZA kuwa ni ajabu au jambo lenye kuzua maswali mengi, lakini ndivyo ilivyo kwamba mastaa wawili wa sinema za Bongo, Irene Uwoya na Hisani Muya ‘Tino’ wanaishi nyumba moja iliyopo, Sinza- Kumekucha, jijini Dar es Salaam, Risasi Jumamosi limenyetishiwa.
Kwa mujibu wa sosi wetu, wawili hao wanaishi kwenye nyumba hiyo tangu Januari mwaka huu baada ya mume wa Uwoya, msakata kandanda Hamad Ndikumana ‘Katauti’, kuondoka nchini na kurudi kwao, Rwanda.
Ndikumana aliondoka nchini kufuatia ndoa yake na Uwoya kuparaganyika kwa kile kilichodaiwa ni kutokuwepo kwa uaminifu na upendo ndani ya nyumba.
Hata hivyo, mtoa habari wetu hakuweka wazi kama ndani ya nyumba hiyo, mastaa hao wanaishi chumba kimoja au kila mtu na chumba chake!
“Mimi ninachojua hawa (Uwoya na Tino) wanaishi nyumba hii, moja! Wanaingia wote na kutoka wote, lakini sijajua kama mle ndani ni kila mtu na chumba chake au la!” alisema mtoa habari wetu.
Aliongeza kuwa, Tino ndiye aliyetangulia kuishi kwenye nyumba hiyo kabla hajafuatia Uwoya mwanzoni mwa mwaka huu.
“Tino ndiye aliyekuwa akiishi pale tangu zamani, ila mwanzoni mwa mwaka huu ndiyo tukamuona na Uwoya naye anaingia na kutoka,” alisema sosi wetu.
Ili kupata usahihi wa madai haya, gazeti hili siku ya Alhamisi iliyopita lilimtwangia simu Irene Uwoya, lakini muda wote kilongalonga chake kiliita bila kupokelewa.
Siku hiyihiyo, Tino alipigiwa simu ambapo alipopokea alisomewa madai yaliyopo mezani kwa gazeti na kutakiwa kutolea ufafanuzi.
“Kwani tatizo liko wapi jamani? Ina maana sisi wasanii hatuwezi kutembeleana au hatuwezi kwenda kwa mtu kukaa na kufanya kazi ya sanaa? Tatizo liko wapi kwani?”
Risasi Jumamosi: Kwa hiyo ni kweli mnaishi nyumba moja na Uwoya?
Tino: Kwani tatizo liko wapi jamani? Sisi hatutakiwi kutembeleana kama kuna kazi za kufanya pamoja?

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...