Monday, August 6, 2012

TUACHE UTANI, TUMUOMBEE WEMA!Wema Sepetu akifanyiwa vipimo katika Hospitali ya Heameda, Upanga jijini Dar.


STAA wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amelazwa katika Hospitali ya Heameda, Upanga jijini Dar akiandamwa na magonjwa ya tumbo na kifua, The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda limeinasa.
Awali kulazwa kwa staa huyo katika hospitali hiyo kulifanywa siri na ndugu zake ambao hawakutaka kuwaambia mapaparazi wa gazeti hili alipo Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006.
CHANZO CHA UGONJWA
Kwa mujibu wa mtu aliyenyetisha habari hiyo, alisema jamii inatakiwa kumuombea Wema kutokana na kuteseka sana na hali ya kushindwa kupumua.
Chanzo hicho kimesema kuwa Beautiful Onyinye amekula vumbi jekundu kwa wingi baada ya kwenda Kigoma hivi karibuni kwenye Tamasha la Kigoma All Stars.
ASHINDWA KUPUMUA
Vumbi hilo jekundu limembana Wema na kumfanya asumbuliwe na tumbo na kubanwa na kifua kiasi cha kumfanya ashindwe kupumua.
HOSPITALI, DOKTA WA DIAMOND
Wema amelazwa katika hospitali hiyo ambayo siku chache zilizopita alikuwa amelazwa kichaa wa Bongofleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na gazeti dada na hili la Ijumaa la wiki iliyopita kuripoti habari hiyo.
Mbali na kulazwa hospitali moja na wodi moja pia daktari anayemchunguza afya Wema ni yuleyule aliyekuwa akimtibu Diamond ambaye anadaiwa kurudisha uhusiano wa kimapenzi na Wema walipokuwa katika ziara hiyo ya Kigoma.
HUYU HAPA WEMA
Gazeti hili lilifanikiwa kupenya katika hospitali hiyo na kuonana ana kwa ana na Wema na kumuuliza kinachomsumbua.
“Kikubwa ni kifua, nahisi kama vile nina pumu, huwa kinanibana na kunifanya nishindwe kupumua vizuri, hata hivyo namshukuru Mungu naendelea vizuri.”
ANA MZIO NA VUMBI
“Kitu kingine siwezi kuvumilia hali ya vumbi, nilipokuwa Kigoma hali hiyo ilinitokea mara kwa mara kwa sababu ya lile vumbi la udongo mwekundu. Kosa nililolifanya nilivyorudi Dar sikucheki afya hadi imefikia hali hii,” alisema Wema kwa tabu.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, Wema alishatoka hospitalini hapo na kurudi kwa mama yake mzazi kwa ajili ya uangalizi wa karibu wa afya yake.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...