Friday, August 17, 2012

NISHA AHONGWA GARI


Gari la Nisha aina ya Toyota Prado.
Nisha akiwa kwenye gari lake.
MSANII kutoka Kiwanda cha Filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amedaiwa kuhongwa gari aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 765 BBT na kigogo mmoja (jina halikupatikana) ikiwa ni siku chache tu baada ya kumwagana na mchumba‘ake, Geofrey.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya kuachana na mchumba’ake huyo na kuvua pete ya uchumba, Nisha alimpata kigogo mmoja wa serikalini ambaye pia ni ‘walewale’ (mume wa mtu) na ndiye aliyemnunulia gari hilo ambalo anatanua nalo mitaani kwa sasa,  huku akiwa  hataki kumuanika mwanaume huyo hadharani.
“Unajua Nisha hataki kumuweka wazi huyo kigogo kwa sababu kwanza ni mume wa mtu, pia ni mtu anayefanya kazi serikalini hivyo kwa kukwepa hilo anadai gari hilo amelinunua jambo ambalo si kweli, ingekuwa sanaa inalipa hivyo, basi wasanii wote wa filamu wangekuwa na magari,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi mapaparazi wetu walimsaka Nisha kwa udi na uvumba na kufanikiwa kumnasa Agosti 13, mitaa ya Sinza, jijini Dar akiwa na gari hilo.

Baada ya kumsomea mashitaka yake yote, msanii huyo mwenye kipaji cha kutembea na waume za watu, alisema:
“Jamani jamani! Hili gari nimelinunua kwa pesa zangu na nimezipata kutokana na filamu ninazouza, nawashangaa mnaponiambia nimehongwa, nimelinunua kwa shilingi milioni 60.
“Wasanii wengi wanasema filamu hazilipi lakini kwangu zinalipa kwani nimepata mafanikio mengi ambayo sikuyategemea, wanaosema hazilipi ni wale wanaoshirikishwa kwenye filamu lakini mimi nacheza za kwangu.”

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...