Friday, August 10, 2012

NILIJUA SITAPONA JAMANI -SAJENTI


Husna Idd ‘Sajenti’.

MNYANGE anayeshikilia ‘taito’ ya Kimwana Manywele 2009 ambaye pia ni msanii wa filamu Bongo, Husna Idd ‘Sajenti’ kutokana na jinsi alivyougua amesema alijua hatapona, Ijumaa liliongea naye.
Sajenti alikuwa kwao mkoani Shinyanga akisumbuliwa na homa ya mapafu, hali iliyokuwa imezua hofu kwa ndugu, jamaa na marafiki zake.
Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kupata nafuu, mwanadada huyo alisema alikuwa akisikia maumivu makali sana kiasi cha kukosa matumaini ya kuendelea kuishi.
“Hali yangu ilikuwa mbaya, kama ni kuugua kwa kweli nimeugua na kulichungulia kaburi, sikujua kama siku moja nitaweza kuwa na hali hii, namshukuru Mungu sasa nina nafuu ila tatizo lililobaki ni kutoona vizuri,” alisema Sajenti.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...