Thursday, August 9, 2012

NDOA YA JACK PATRICK CHALI


Imelda Mtema na Shakoor Jongo
KWA mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wanandoa hao, ndoa hiyo ilisambaratika mara tu baada ya mume wa Jack kuswekwa rumande Keko, Dar kwa tuhuma za usafirishaji wa mihadarati.
UTATA WA CHANZO
Chanzo hicho kilitiririka kuwa ndoa hiyo inadaiwa kupigwa bomu na kusambaratika kutokana na mambo ambayo yanaendelea kati ya wanandoa hao.
Kilidai kuwa tangu Tiff awekwe nyuma ya nondo, ndipo mambo yalipokwenda kombo kutokana na  kitendo hicho kumuumiza Jack.
JACK KUSHANGAZA WATU
Baada ya madai hayo mazito kutua kwenye dawati la Amani, waandishi wetu walimtafuta Jack na kumuuliza kama ni kweli ndoa yake imevunjika ambapo hakutaka kuzungumza chochote ila alipobanwa zaidi akadai kuwa siku mumewe akitoka ndiyo atatoboa mambo mazito yatakayowashangaza watu wengi juu ya ndoa yake.

SHANGAZI
Amani lilimsaka shangazi wa Tiff ambaye aliomba hifadhi ya jina kwa kuogopa kufanyiwa fujo na wawili hao pindi jamaa atakapotoka mahabusu ambaye alisema kuwa matatizo hayo yote yaliyomtokea Tiff aliyataka mwenyewe kwani Jack alikubali kuolewa kufuata fedha na si kwa mapenzi.

SHANGAZI ANATIRIRIKA
“Haiwezekani mtu akataka kufunga ndoa na wewe halafu unampa masharti kuwa huhitaji michango kwenye harusi yako na kudai unataka ndoa yako iwe ya kifahari, hapo kuna ndoa kweli? Matokeo yake Tiff kapata matatizo na wa kumhurumia hakuna,” alisema shangazi huyo na kuongeza:
“Tulijua mapema tu kuwa pale hamna ndoa. Cha msingi Tiff atamke tu wazi kuwa hakuna ndoa ndipo tujitokeze.”

TIFF
Wiki mbili zilizopita, Tiff aliliambia gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda kuwa ni kweli tangu atiwe mbaroni Jack hajawahi kwenda kumuona mahabusu.

ILIGHARIMU SH. MILIONI 75
Jack na Tiff walifunga ndoa ya kifahari kwenye Ufukwe wa Coral Masaki, Dar na kufuatiwa na sherehe kubwa kwenye Ukumbi wa Hoteli ya The Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro (zamani Kilimanjaro Kempinsk), na kugharimu Sh. milioni 75, bila mchango kutoka kwa mtu yeyote.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...