Friday, August 17, 2012

MZEE AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA BASI LA ‘UPENDO’ MJINI MOROGORO


Askari wakiushusha mwili wa mzee Petro Michael kutoka kwenye basi la Upendo.
Mwili wa Mzee Petro baada ya kutolewa kwenye basi.
Askari wakiangalia tiketi aliyokuwa nayo marehemu.
Mwili wa marehemu Petro, pembeni yake ni hela yake aliyokuwa nayo shilingi 4,000/=.
Basi la Upendo alimokuwa marehemu Petro.
---
MZEE mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Petro Michael, aliyekuwa akisafiri na basi la Upendo kutokea Mbeya kwenda  Dar es Salaam amekutwa amekufa  ndani ya basi hilo mjini Morogoro.
Akizungumza na mtandao huu, Michael Paul, dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T415 BBA alisema waligundua mzee huyo amekufa walipofika stendi ya mabasi ya Msamvu mkoani  Morogoro  ambako mzee huyo  alipaswa kushuka.
"Tulipofika Mikumi mzee huyu alimkumbusha kondakta wangu kwamba anashuka Msamvu,  hivyo tulipofika Msamvu konda alifika kwenye siti ya mzee huyo kwa lengo la kumtaka ashuke.  Cha ajabu alipofika pale alimkuta ameshakufa hivyo tukaamua kuja hapa polisi, " alisema dereva wa gari hilo kituo cha polisi ambako basi lilikwenda na abiria.
Baadhi ya abiria wa basi hilo waliokuwa jirani na mzee huyo ndani ya basi  walipohojiwa na mtandao huu walisema  mzee huyo ambaye afya yake ilionekana kudhoofika alichangiwa  na abiria hao  pesa ya kula waliposimama kupata chakula njiani.
Mwili wa mzee huyo umehifadhiwa Hospitali ya Mkoa Morogoro ambako ndugu zake wanaweza kwenda kuutambua.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...