Wednesday, August 1, 2012

Msanii maarufu Somalia auawa Mogadishu


Msanii Marshale auawa Somalia
Msanii mchekeshaji maarufu nchini Somalia ameuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake mjini Mogadishu ba watu wawiliwasiojulikana. Mpiango ya mazishi inaendelea.
Abdi Jeylani Marshale alikuwa maarufu kwenye vipindi vya televisheni na redio na inaarifiwa kuwa alikufa baada tu ya kumtoka kwenye kituo cha redio.
Haijajulikana nani anahusika na mauaji hayo lakini mwaka jana alitishiwa na wapiganaji wa al-Shabab.
Alikuwa akichekesha watu kuigiza kama wapiganaji wa kiislam.
Walioshudia wameiambia BBC kuwa Marshale alipigwa risasi mara kadhaa kichwani na kifuani ba watu waliokuwa na bastola.
Baada ya kutishiwa na al-Shabab, alikwenda eneo jirani la Somaliland siku kadhaa baada kabla ya kurudi nyumbani.
"Siku ya huzuni leo kwenye tasnia ya sanaa na burudani, alikuwa kiongozi wa sanaa ya uchekeshaji na kila mtu alipenda kazi yake. " alisema Yusuf Keynan, mtangazaji wa Redio ya Kulmiye ambako Marshale alikuwa akifanya kazi.
Wakati huo huo inaripotiwa kuwa watu wawili wamejilipua nje ya lango la bunge mjini Mogadishu, na kumuua askari wa serikali na wao wenyewe.
Afisa wa polisi ameaambia waandishi wa habari kuwa watu hao walijilipua baada ya askari wa polisi kuwafyatulia risasi. Hakuna kundi lolote lilijitokeza kuhusika na shambulio hilo.
Tukio hilo limetokea wakati viongozi wa Somalia wakijadili juu ya katiba mpya ya nchi hiyo.
Vikosi vya Umoja wa Afrika na serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa vimelitimua kundi la al-Shabab nje ya Mogadishu lakini kundi hilo lenye uhusiano na al-Qaeda mara nyingi limefanya mashambulizi katika mji huo.
Bado linadhibiti maeneo mengi kusini na katikati mwa Somalia.
Somalia haijawa na serikali thabiti tangu mwaka 1991.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...