Saturday, August 4, 2012

Mke: BABY MADAHA KANIPORA MUMEMKE wa mwigizaji wa filamu Bongo, Slim Omar, Khadija Amir ‘Kay’ (pichani  juu) amemfungukia msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ kuwa amempora mume.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar, Khadija alidai kuwa alimwagwa na Slim huku akiwa mjamzito na kwenda kupiga kambi kwa Baby Madaha.
“Mimi nalia na Baby Madaha jamani. Amenipora mume wangu, Slim. Mbaya zaidi aliniacha nikiwa na ujauzito kama hivi mnavyonioa. Lakini sijali kwa sababu naamini kama sikupangiwa niishi na Slim hata nikifanya nini haitasaidia.
“Nashangaa sana kufanyiwa kitu kama hicho na mtu ambaye ni rafiki yangu wa siku nyingi, bora angefanya mwingine lakini si Baby Madaha,” alisema Khadija ambaye ni Miss Shinyanga 2009.
Baby Madaha anayelalamikiwa kwa ‘wizi’ wa mume, alipopatikana kwa njia ya simu alisema yeye hayupo tayari kuzungumzia mambo yasiyo na msingi zaidi ya kutafuta fedha.
“Slim kweli namjua, nafanya naye kazi. Juzi tu hapa nilikuwa nashuti naye wimbo wangu mpya, ghafla ndiyo huyo mwanamke (Khadija) akaanza kunitukana na kudai nimemuibia mumewe.
“Sasa kama anadai wameachana anachokitafuta tena ni nini? Si amuache Slim awe huru kutafuta mtu mwingine?” alisema Baby Madaha pasipo kuweka wazi kama wanatoka na mwanaume huyo au vipi.
Jitihada za kumpata Slim ili kufafanua juu ya msimamo wake kwa wanawake hao hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...