Thursday, August 2, 2012

MAMBO MUHIMU JUU YA MAJINA YA TOVUTI (DOMAIN NAMES)


Katika dunia ya leo internet ni kitu muhimu kwa maisha ya kila siku,sio tu kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kazi bali hata kwa kuongeza mahusiano kati ya wanajamii. Vilevile makampuni mengi yamekuwa yakitumia internet kama sehemu muhimu ya kufanyia biashara.Wengi wetu tumekuwa tukitajataja majina au anuani za tovuti nyingi kama afroit,google,baidu nk kwa urahisi,wapo ambao hatufahau kwanini baidu na si google,kwanini haya majina ni ya kipekee na hayafanani.Hayo yote ndio yanaitwa domain name. Leo,mdau atafafanua domain names kwa undani na kukupa mdidi tosha,tutaweza kujua ni nini Domain name,kwanini tunatumia,faida za kutumia na mambo ya kuzingatia kabla ya kuchagua Domain name. Domain name ni nini?
Kila kitu kilichopo kwenye internet kina asili au chanzo chake kinapotoka,ambayo hutambuliwa kwa kutumia muunganiko wa kanuni na sheria nyingi,kwa lugha za kiufundi hujulikana kama Uniform Resource Locator (URL).Domain name ni sehemu ya hii anuani(URL) ambayo hupewa kila tovuti au seva iliyopo kwenye internet ili kujitofautisha au kujitambulisha kwa nyingine.
Mfano mzuri wa Domain name ni “www.afroit.com”.Inasomwa toka kushoto kuelekea kulia,www inasimama badala ya world wide web,halafu afroit ni jina la mmiliki,vilevile kuna wakati unaweza kukutana na Domain name za daraja 
la pili,mfano blog.afroit.com hapa “blog” ni domain ya daraja la pili ambayo imesajiliwa na kampuni au tovuti ya AfroIT.
Kulia kabisa utakuta kuna “com” ambayo tunaiita domain level daraja la kwanza,mara nyingi huwakilisha dhumuni la tovuti au kampuni au mdau anayemiliki domain.Tukiangalia kwa undani utaona Domain za daraja la pili ni kama motto wa mmiliki wa Domain name.Hizi domain za daraja la kwanza domain namezimegawanyika kutegemeana na dhumuni au malengo ya kampuni,tuangalie michanganuo mbalimbali ya hizi domain za daraja la kwanza.
.com  Humaanisha biashara au huduma iliyokaa kibiashara(commercial),hivyo kama unataka kusajili tovuti ambayo itatumika kwa matumizi ya kibiashara basi .com ndio chagua malidhawa.Ingawawamiliki wa tovuti nyingi zimekuwa zikikimbilia .com kutokana na umaarufu na mazoea ya .com kulinganisha na domain nyingine za daraja la juu.
.gov/go  Kwa ajili ya matumizi ya kiserikali,tovuti yoyote ambayo haina uhusiano au si ya serikali hairuhusiwi kutumia domain name zenye .gov,mfano wa website zenye .go ni kama http://www.tanzania.go.tz.
.edu/.ac  Kwa ajili ya matumizi ya kielimu,mfano mashule,vyuo,nk ,www.udsm.ac.tz auwww.znufe.edu.cn   ni baadhi ya mifano dhahiri.
.org  Kwa makampuni au mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo hutoa huduma kwa jamii(NGO),kwa mfano http://plan-international.org/ vilevile hutumiwa na makampuni au taasisi ambazo mara nyingi huwa haziwezi kuingia kwenye makundi mengine ya domain daraja la kwanza
.net  Kwa wanaotoa huduma za internet,kwa mfano http://www.telecomcareers.net/
Na nyingine nyingi ambazo hazitumiki kwa wingi,hivyo ni muhimu kuzingatia dhumuni na malengo ya kampuni au taasisi kabla ya kusajili Domain name.
Ili kuweza kurahisisha utambulishi,Domain name pia huweza kusajiliwa kutegemea na mgawanyo wa kijiografia.Kwa mfano hapa Tanzania tunatumia .tz ikimaanisha Tanzania,kenya wanatumia .ke wakani China wanatumia .cn ikimaanisha China.
Kampuni iliyopo Tanzania inaweza kusajili Domain ya kwanza kama .com vilevile inaweza kusajili kama.co.tz. Kwakuwa Domain za kwanza(top level Domains)hushughulikiwa na InterNic ambayo huwa haiangalii mgawanyiko wa kijiografia, hivyo kila domain ya kwanza hutambulika kiupekee,mfano kama Domain name ya afroit.com tayari imeshasajiliwa,basi Domain name hiyo haiwezi kusajiliwa na mtu mwingine yeyote ili kuondoa muingiliano wa domain.Hii inarahisisha kazi kwa makampuni yanayofanya biasha za kimataifa ambayo hutumia Domain moja dunia nzima.

Jinsi Domain name inavyofanya kazi

Dhumuni kubwa la domain name ni kurahisisha utambuzi wa tovuti.Yao husimama badala ya anuani ya IP, kwa mfano  IP address yenye anuani kama “193.45.0.9″ huweza kuwakilishwa na domain name ya tanzmed.com..Hivyo basi badala ya mtumiaji kuandika namba ambazo ni ngumu kukumbuka basi anaandika Domain name,baada ya hapo kuna kompyuta za kiwango cha juu(DNS Server -Domain Name System Server) hufanya kazi za kutafsiri domain kwenda IP address halafu kuunganisha maombi kwenda kwa kompyuta husika,kama fundi mitambo wa TTCL anavyounganisha simu vile.
Faida kubwa ya kutumia domain name ni kuwa,haiitaji kubadilika hata kama anuani ya IP inayowakilisha kompyuta au seva itabadilika,kumbuka kuna sababu nyingi zinawweza kukupelekea kuhitaji kubadilisha anuani ya IP,ikiwemo kuhama toka kwa mtoa huduma mmoja kwenda kwa mwingine. sasa basi, hata kama itatokea mbadiliko wa anuani yaIP,bado watumiaji wako basiwataendelea kukupata,kwani wengi wao hata hawatojua kama anuani yako ya IP imebadilika,huo ndio msaada ya domain name.katika mabadiliko kama haya,kinachofanyika ni kubadilisha muunganisho wa Domain name na IP ili kuunganisha kwenye IP mpya. Ni ukweli usiofichika kuwa Domain name inaleta mdidi kulinganisha na uchominambavu ambayo ipu kwenye IP address.

Jinsi ya kuchagua Domain name

Kama tulivyoona,Domain name ndio utambulishi wa tovuti yako kwenye Internet,hivyo uchaguzi wa Domain name ni lazima ufanyike kwa kuzingatia mambo mengi,ni ngumu kuyafafanua yote hapa ila nitakueleza kwa uchache tu kama ifuatavyo

 Domain name yako iwe website yako

Domain name ni lazima iendane na website yako,hivyo kuleta maana tosha ya website,kwa mfano mtu akisikia AfroIT  kichwani kunakuja picha ya mambo mawili Africa na IT,hivyo haimpi tabu kuyakinisha shughuli au lengo la tovuti

    Rahisisha domain yako

   Kwa mfano wewe ni muuza magari,sasa unafikiria website yako kuiita magari.com  au kutumia brand mojawapo ya magari yako mfano mikweche.com ambapo mikweche ni brand mojawapo,mara nyingidomain ya pili inaleta maana zaidi kwani inakuwa ya kipekee zaidi.

 Tumia Domain fupi

Lengo la domain nikurahisisha kazi au kumuwezesha mtumiaji kukumbuka kwa urahisi,hivyo kutumia domain ndefu kunaweza kuwaletea watumiaji matatizo ya kukumbuka,ingawa kuna majadiliano kuhusu matumizi ya domain defu au fupi,ila binafsi bado nashauri matumizi ya domain fupi,mfano domain kama ibm.com ni rahisi kukumbukika ukilinganisha na Microsoft.com,leo hii website nyingi za china wanapendelea kutumia namba,mfano 126.com m18.com nk ambapo ni rahisi zaidi kukumbukika kwao.

.Com,org,net.etc?

Kama umenisoma hapo juu nimeongelea umuhimu wa kutumia domain kulingana na dhumuni la website,hii ni kweli ila kuna wakati inaweza kukuletea matatizo fulani,ni wangapi wamekuwa na mazoea ya kutumia .net? mfano ingekuwia vigumu vipi kama ungetakiwa kutumia afroit.org badala ya afroit.com? hivyo hili swali nalileta kwenu wadau kwa majadiliano.Uzoefu unaonesha website nyingi zimekuwa zikikimbilia .com ili kuweza kuondoa ugumu wa kukumbuka domain zenye viunganishi zaidi ya .com
Kwa kumalizia zingatia yafuatayo

 Asilani:

  Usipanic!
  Epuka kutumia alama za ajabu ajabu kwenye domain,kama afro!t.com .
 Epuka kutumia, ’2′ukimaanisha ‘to’, ’4′ ukimaanisha ‘for’, ‘u’  ukimaanisha ‘you’.
 Epuka kutumia brand names au trade marks za kampuni nyingine(tutaongelea hili kwenye mada zijazo),sio tu unaweza kushtakiwa,bali inaweza kukupelekea kufunikwa pindi hiyo brand nyingine ikiwa ni kubwa na maarufu zaidi yako.

       Mara zote:

  Hakikisha ni rahisi kuikumbuka.
  Hakikisha ni rahisi kuitamka kwa simu.
  Tumia lugha rahisi
  Tumia maneno yenye maana
  Tumia  search engine keywords. (tutaongelea siku za usoni)
  Chagua domain provider mwenye uhakika. Usiwe tayari kuongopewa au kurubuniwa.
Hivyo uwanja upo wazi,ongezea orodha hizi…

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...