Friday, August 10, 2012

BABY MADAHA KWISHA KAZI, ALEWA AANGUSHA GARIWADAU mbalimbali wamemtahadharisha msanii wa filamu ambaye pia anafanya muziki, Baby Joseph Madaha kupunguza kunywa pombe kwani asipojiangalia itamuua.
Hayo yamekuja kufuatia msanii huyo kunaswa na paparazi wetu maeneo ya Kinondoni jijini Dar akiwa bwii huku mkononi ameshikilia chupa ya pombe kali.
Akiwa maeneo hayo, Madaha alionekana kuzidiwa na kilevi hicho, kitendo kilichowafanya vijana wa kihuni kumzengea ili kama angezima jumla wamfanyizie.
Hata hivyo, baada ya msanii huyo kubaini kama angejipindua tu wahuni wangemfanyia mchezo mbaya, aliamua kujikokota na kwenda kujichanganya kwenye kundi la wasichana wengine.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...