Tuesday, August 7, 2012

AUA MKEWE NA KUMLA NYAMA!


Mtuhumiwa wa mauaji, Jiemng Liu.
BABU mmoja mwenye umri wa miaka 79, Jiemng Liu  ameshitakiwa mahakamani nchini Uingereza kwa kosa la kumuua mkewe na kumla nyama yake.
Mwendesha mashitaka katika mahakama moja ya Wilaya ya Westbrough nchini humo aliiambia mahakama hivi karibuni kuwa Liu alikutwa ameketi kwenye kiti cha magurudumu katika makazi yao Mtaa wa Shrewsbury akiwa ametapakaa damu ya mke wake aitwae Yuee Zhou (73) mdomoni, mikononi na puani ambaye alikuwa amemuua.
 Liu tayari ameshitakiwa kwa kosa la mauaji ya mkewe huyo. Akiwa katika mahakama hiyo ya wilaya, babu huyo alifikishwa mahakamani akiwa amevaa pajama nyeupe na miguuni akitembea pekupeku.
Hata hivyo, kutokana na madai kuwa alikutwa akiwa amemuua mkewe na akawa anakula nyama yake, mahakama iliamuru apelekwe hospitali ya magonjwa ya akili ili akapimwe ubongo wake kama yupo sawasawa au la kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi yake.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...