Watu 54 wamefariki dunia wakati 
wakijaribu kuvuka bahari kutoka Libya kwenda Italia kwa kutumia boti la 
mpira wa kujaza pumzi, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa 
linalohusika na masuala ya wakimbizi.
Mtu pekee aliyenusurika balaa hilo, aliyeokotwa 
na wavuvi kutoka Tunisia,amesema kuwa wenzake walizama kutokana na kiu 
baada ya kusafiri kwa zaidi ya siku kumi na tano baharini.
Ameliambia
 shirika la UNHCR kuwa walikaribia pwania ya Italia lakini wakasumbuliwa
 na mawimbi makali yaliyowasukuma hadi boti lao lilipoishiwa na pumzi.
Inasadikiwa kuwa wengi wa watu hao ni kutoka Eritrea.
Manusura ambaye ni raia wa Eritrea pia, 
aliokolewa na wavuvi wa Tunisia nje ya pwani ya Tunisia na kwa wakati 
huu anatunzwa kwenye hospitali ya nchini Tunisia.
Aliliambia shirika la UNHCR kuwa kundi la watu 55 liliondoka Libya mwishoni mwa mwezi Juni.
Manusura huyu aliendelea kumfahamisha msemaji wa
 Umoja wa Mataifa Laura Boldrini kuwa "matatizo yalianza punde baada ya 
kuvua nanga, na kwa bahati mbaya hatukuruhusiwa kuchukua hata chupa moja
 ya maji ya kunywa, kwa hiyo tulipokosa njia na mwendo wetu kuendelea 
watu wakaanza kujihisa wagonjwa na kufariki kutokana na kukosa maji.
According to the UNHCR, around 170 people have died this year trying to reach Europe from Libya.
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia 
masuala ya wakimbizi,UNHCR limesema kuwa hadi watu 1,300 wamefanikiwa 
kuvuka hadi Italia kupitia bahari tangu kuanza kwa mwaka huu 2012.
Raia wengi wa Eritrea hujaribu kila njia ili kufika sehemu yoyote ya Ulaya au Israil kutafuta maisha bora.
Wakosoaji wanasema wanaikimbia serikali dhalimu 
inayowakandamiza, umasikini na kulazimishwa kujiunga na Jeshi la Taifa 
wanapotimizia umri wa miaka 40.
No comments:
Post a Comment