BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Friday, July 13, 2012

Uchumi wa China waanguka na kuleta hofu

Uchina imeandikisha ukuaji wa uchumi mdogo zaidi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Uchumi wa china washuka
Kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa na serikali ya nchi hiyo, uchumi wa uchina ambao ndio wa pili kwa ukubwa duniani ulikuwa kwa asilimia saba nukta sita katika robo ya pili ya mwaka huu, hii ikiwa ni asilimia moja nukta nne chini ya kiwango kilichoafikiwa katika robo ya kwanza mwaka huu.
Kuanguka huko kwa uchumi kunasemekana ni sababu ya kupungua kwa mauzo ya nje na watu kubana matumizi yao ndani ya China.
Mwandishi wa BBC mjini Beijing anasema kuwa viongozi wa china wameweka matumaini yao katika kuvuta uwekezaji mpya ili kuchochea kukuwa tena kwa uchumi.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...