
Bradley Wiggins amekuwa
Muingereza wa kwanza kushinda mashindano ya baiskeli ya Tour de France
huku Mark Cavendish akifanikiwa kutawala hatua za mbio hizo kwa siku nne
mfululizo.
Wiggins mwenye umri wa miaka 32 alimalizia
mashindano hayo katika mitaa ya jiji la Paris kwa ushindi mwembamba wa
dakika tatu na sekunde ishirini na moja.
Mwanatimu
mwenzake kutoka timu ya Team Sky, ya Uingereza Chris Froome alishikilia
nafasi ya pili na Vincenzo Nibali wa Italy nafasi ya tatu.
Cavendish alitawala hatua ishirini na tatu za mashindano hayo.
Hii ilimfanya kumpita mshindi wa mara saba wa
mashindano hayo Lance Armstrong na Mfaransa Andre Darrigade ikiwa ni
mara kumi na moja pungufu ya Eddy Merckx wa Ubelgiji aliyekuwa na rekodi
ya 34.
''Inapendeza sana,'' asema Cavendish. ''Haingeweza kuwa zaidi ya hapo,kwani ni mashindano ya kuvutia sana kwetu.
''Inafurahisha, miaka minne iliyopita lengo lilikuwa ni kushinda jezi za njano na tumefanikiwa.
''Tuna kazi moja zaidi ya kufanya wiki ijayo katika mashindano ya Olympics, na itakuwa wiki chache za kufurahisha kwetu.''
Lakini siku hii ni maalum kwa Wiggins ambaye kwa
uangalifu kabisa alipita mitaa ya Paris kukamilisha taratibu rasmi za
mashindano hayo baada ya ushindi wa kushangaza wa majaribio siku ya
Jumamosi kumpatia mafanikio yasiyopingika.
Bingwa huyo wa mara tatu wa Olympic alishuhudiwa
na watu waliokuwa wakimshangilia baada ya kumuwekea mazingira mazuri
Cavendish katika mbio hizo mbele ya maelfu ya mashabiki wa kiingereza
waliojitokeza kushuhudia ushindi huo wa kihistoria.
No comments:
Post a Comment