BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Wednesday, July 11, 2012

MSANII WA FILAMU AFANYA MADUDU MBELE YA MAMAKE MZAZI







CHIPUKIZI anayekuja kwa kasi kwenye soko la filamu Bongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ kwa mara nyingine anatengeneza kichwa cha habari baada ya kufanya uchafu huku akishuhudiwa na watu, Risasi Mchanganyiko linakufunulia.
Madudu ya Vai yalinaswa laivu na kamera yetu, wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Motema uliopo Mwananyamala, Dar ambapo kulikuwa na ‘birthday’ ya msanii huyo.
Mbele ya macho ya watu, bila kujali kuna waliomzidi umri, Vai alikuwa karibu sana na mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Boniface ambaye alitambulishwa kama boyfriend wake na kuanza kudendeka naye bila aibu.
Aidha, kuna wakati alikamatana na baadhi ya rafiki zake wa kike na wa kiume (wanaodaiwa ni kuku watamu) na kuanza kudendeka kama alivyofanya kwa Boniface.
Kama hiyo haitoshi, Vai alifikia hatua ya kupandisha gauni lake juu na kuacha ‘kufuli’ lake nje kama vile alikuwa bafuni (angalia picha ukurasa wa nyuma).
Watu wenye heshima zao walibaki vinywa wazi na kugeuza nyuso kukwepa aibu ya msanii huyo ambaye anaonekana kuamini kufanya uchafu ndiyo kupata ustaa.
MAMA ASHUHUDIA
Mambo yote hayo yalifanyika huku mama yake mzazi ambaye alikuwa mmoja wa waliohudhuria, aliyetambulishwa kwa jina la Anna Thomas akishuhudia.
Baada ya kuona mwanaye anazidi ‘kumvua nguo’ kwa kufanya matendo ya hovyo, mama huyo alimkemea kuacha kuendeleza mfululizo wa matukio ya kuchefua lakini ikawa ndiyo kama amempulizia filimbi ya kuanza.

AMJIBU MAMA’KE
Wakati mama yake akimfokea na kumtaka aache kufanya uchafu, yeye alitoa kauli ya hovyo iliyoonekana ni kama alimjibu mama yake.
Vai alisikika akisema: “Acheni nijiachie leo ni siku yangu ya kuzaliwa na nimetimiza miaka 18 sasa kuna kitu gani nitazuiwa tena?”

MASWALI TATA YA KUJIULIZA
Ikiwa msanii huyo ndiyo alikuwa akitimiza umri wa miaka 18, ilikuwaje akawa na mpenzi kabla ya kufikisha umri huo?
Kama aliweza kufanya vitendo vya chumbani na mpenzi wake aitwaye Boniface mbele ya mama yake, inawezekana mama huyo alikuwa akiutambua uhusiano huo? Kama ndivyo, kwa nini hakukemea akijua mwanaye bado mtoto?


1 comment:

  1. Nice blog here! Also your site loaԁs up very fast!
    What host аre уou uѕing? Can I get уour аffiliate link to your
    host? I wish my websіte loaԁed up as quickly as yourѕ lol

    Мy homepage ... payday loans
    Also see my web site: payday loans

    ReplyDelete

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...