BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Tuesday, July 31, 2012

HUYU NDIO WAZIRI MKUU ALIEMPIGIA KURA PREZZO KWENYE BIG BROTHER AFRICA.


Raila Odinga akiwa anampigia Prezzo kura na picha akaiweka kwenye page yake ya twitter yenye watu zaidi ya elfu 67.
Jaribu kufikiria kama ni wewe ndio ungekua umeshiriki shindano la Big Brother Africa alafu ukapigiwa kura na Waziri mkuu wa nchi yako tena kura ambayo ametangaza hadharani ikiwa imebaki wiki moja tu game kumalizika.
Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amekua kiongozi wa juu wa nchi mimi kuona ushahidi wake wa kumpigia kura mshiriki wa shindano la Big Brother Africa ambalo baadhi ya viongozi wakuu wamenukuliwa kwenye vyombo vya habari kwamba hawaliungi mkono.
Jumatatu July 30 2012 Raila Odinga alikwenda kwenye page yake ya twitter iliyo verrified na kuandika kwamba tayari amepiga kura yake kwa Prezzo ndani ya Big Brother kwa kutuma sms.
Shindano la Big Brother linatarajiwa kumalizika July 5 2012 ambayo ni jumapili ijayo, ambapo mpaka sasa Prezzo ndio anaongoza kwa kupigiwa kura nyingi za swali wanaloulizwa watu ni Mshiriki gani wanaetaka ashinde.. chek hapo chini.
Hizi ni kura za July 31 2012 saa tisa kamili usiku wa kuamkia July 31, Prezzo wa Kenya ndio anaongoza kama unavyoona hapo juu anafata Lady May ni wa Namibia, Keagana ni wa South Africa, Kyle ni wa Uganda, Talia ni wa Zambia na Wati ni wa Malawi.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...