
DEMU mwenye makuzi ndani ya tasnia ya filamu bongo Christine John 
‘Sintah’ aka J LO wa Bongo, inadaiwa kuwa kwa sasa wenda akakosa kabisa 
marafiki kwani tabia yake ya kujiona na dharau ndiyo inasababisha wengi 
kumkibia.
Chanzo kimoja cha habari kilichozungumza na mwandishi wa DarTalk ambaye 
hakutaka jina lake litajwe, alidai kuwa msanii huyo amekuwa na urafiki 
na watu maarufu huku akisahau kuwa hao wanaweza kumkimbia muda wowote 
endapo akiishiwa.
Chanzo hicho kilisema kuwa wiki iliyopita alitofautiana na mmoja kati 
marafiki zake wakubwa na hali hiyo ndiyo inayosababisha hata wale 
wengine kuhisi kuwa mwanadada huyo ni mtu asiye na upendo kwa wengine 
kutokana na tabia yake ya kujiona.
“Wiki iliyopita tu katofautiana na msanii mwenzake naweza kumtaja jina 
lakini itakuwa si vizuri, hivyo yupo katika wakati mgumu kwani ana 
majivuno mno na kuna time anakera sana kwa tabia zake za kujiona yuko 
juu zaidi ya wengine,” Kilidai chanzo hicho.
Katika harakati za kumtafuta Sintah ili aweze kujibu mapingo ya 
kutofautiana na mwenzake na kukimbiwa na marafiki, alijibu kuwa hiyo 
haimuhusu mtu kwani anaishi maisha yake na hana bifu na mtu hivyo haoni 
kama kuna mtu anaweza kumtisha kwa lolote.
“Huyo aliyekupa hizi taarifa ungemwambia akutajie na jina la huyo msanii
 nilitofautiana naye, sasa kwanini unaniuliza mimi, kwanza suala la mimi
 kukimbiwa na marafiki yeye linamuhusu nini kama si matatizo aliyonayo,”
 alijibu.
Pia demu huyo aliongeza kuwa kwa upande wake hana urafiki na watu au 
wasanii wale wasiojishungulisha na kazi ama biashara nyingine nje ya 
filamu.
 
 

No comments:
Post a Comment