Kama unakumbuka Siku 49
zilizopita, Mwimbaji wa zamani wa Bongo fleva ambae sasa ni mwimbaji wa
nyimbo za Injili Stara Thomas kupitia AMPLIFAYA alitaja sababu za yeye
kushindwa kufanya kolabo na wasanii wengine wa gospel kwenye album yake
mpya na ya kwanza toka aokoke mwaka mmoja uliopita.
Alisema “kwenye upande wa
Injili waimbaji wengi bado hawajawa na ufahamu wa kufanya kolabo japo
lile ni neno la Mungu linalosimama peke yake haijalishi mnashirikiana au
hamshirikiani lakini kushirikiana ni jambo jema, ugumu ambao nimeuona
na nimejifunza ni kuhusu unafiki mkubwa sana, mtu anaweza kukuchekea
machoni lakini moyoni ni muongo, kuna wengine wasanii wakubwa niliwaona
nikafikiri lakini nilipowakaribia nikagundua sio, unafiki ni mwingi,
kule kwenye bongofleva kulikua kuna upendo”
.Baada ya hayo, Mchungaji
mtarajiwa ambae pia kwa sasa ni mwimbaji wa nyimbo za injili pia,
mchekeshaji Masanja Mkandamizaji wa Orijino Komedi amekubali kutoa wazo
lake kuhusu ishu ya Stara kukosa ushirikiano wa kutosha kwa wasanii wa
Gospel aliowategemea.
Hii ndio kauli yake….. “Hii
kazi inayofanyika huku kwenye Gospel ni huduma sio biashara, hii ni
huduma tunayoifanya kwa hiyo mwanadamu yeyote, wito kwa Stara na wasanii
wengine wanaotoka kwenye bongofleva na kuja kwenye Gospel na kukutana
na hivi vitu, ulichofata kwenye Gospel sio kolabo na flani, umefata
kufanya huduma ya wewe na Mungu wako fanya hiyo kwa sababu hata
usiposhirikia na na mtu bado kazi yako ikifanywa mbele za Mungu
itahesabiwa haki, umeokoka ili umtumikie Mungu.. mtumikie uachane na
binaadam kwa sababu sio wote wanaoimba Gospel wanamcha Mungu, kuna
mwingine anaimba Gospel kama biashara sasa ukisema mshirikiane akakataa
itakuumaje na wewe unamtumikia Mungu?”
Hii sio mara ya kwanza kwa
wasanii waliotoka kwenye bongofleva mpaka kuokoka na kufanya muziki wa
Gospel kutoa hayo malalamiko, mwigizaji Dokii pia alishawahi kuwachana
sana na kusema wasanii watano wakubwa wa Gospel Tanzania hakuwataja kwa
majina lakini alisema ndio wanafiki wakubwa, wana ubinafsi, chuki,
kujisikia na kujitenga na hawakukubali kumpa ushirikiano wowote.
Waimbaji wa Gospel wenyewe
wameshawahi kukiri kwamba hakuna upendo kati yao, watu wanachukiana,
hawana umoja.. Rose Muhando, Upendo Nkone na Miriam Mauki walishalisema
hilo kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM.

No comments:
Post a Comment