TV STAR KIM KARDASHIAN HAJUI ANGEMUELEZAJE BABA YAKE.
Reality Tv star Kim Kardashian
amesema hajui angemuelezaje baba yake mzazi kuhusu mkanda wa picha
nyeusi aliorekodi na boyfriend wake wa zamani R’n'B star Ray J.
Baba mzazi wa Kim, Robert Kardashian alikua mmoja wa wanasheria wakubwa Marekani na alifariki kwa ugonjwa wa kansa mwaka 2003.
Kwenye mazungumzo yake na
mtangazaji Oprah, Kim ambae ni wife to be wa Kanye West amesema ingekua
ngumu kuzungumza na baba yake kuhusu hiyo ishu likiwa ni kosa ambalo
alilijutia kufanya pia.
Kuhusu kuachana na mume wake
ambae ni basketballer Kris Humphries waliekaa kwenye ndoa kwa siku 72 tu
staa huyu wa Keeping up with the Kardashians amesema mwanzoni
walipokutana na kuanza mahusiano ilikua ndani ya muda mfupi sana mpaka
wakafunga ndoa, hawakuwahi kukaa pamoja zaidi ya wiki moja kabla ya
kufunga ndoa ila walipooana ndio akajua Kris hakua aina ya mwanaume
anaemtaka.
No comments:
Post a Comment