TUJIFUNZE KUHUSU MAPENZI
UKWELI KUHUSU KUPENDA, KUPENDWA NA KUPENDANA!
TUJADILI pamoja; Unafahamu nini kuhusu mapenzi? Najua majibu ni
mengi, kuna wengine watasema mapenzi ni kupendana...mapenzi ni hisia
kutoka kwa mtu kwenda kwa mwingine n.k. Kuna wakati nilishawahi
kufafanua maana ya mapenzi.
Ngoja niwaambie rafiki zangu. Kwa tafsiri yangu, mapenzi ni hisia za ndani kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine, hisia hizi ili ziwe sahihi ni lazima zigongane ndipo neno UPENDO huanzia hapo.
Kwa maneno mengine, wawili hawa lazima wote wawe na hisia sawa ndipo wapendane. Tunapokuja kwenye mapenzi sasa, inawapasa watu hawa wawe wa jinsia tofauti – mwanamke na mwanaume. Muunganiko wa wapenzi hawa hulenga kujenga maisha ya pamoja. Upo hapo rafiki yangu?

Yes!
Mapenzi ni maisha. Kwa hakika maisha yetu hayawezi kukamilika bila
kuwepo mapenzi. Ninapozungumza juu ya mapenzi namaanisha yale yanayotoka
moyoni kabisa. Si maigizoIkiwa upo katika uhusiano na mpenzi
ambaye hakupendi, yaani wewe peke yako ndiyo unayempenda, wewe ni MTUMWA
WA MAPENZI. Kama ndivyo, kwa nini uwe mtumwa?
Unadhani hakuna mwingine ambaye anaweza kukupenda kwa mapenzi ya dhati na penzi hilo likawa kwa pande zote? Inawezekana, huna sababu ya kulazimisha penzi kwa mtu ambaye hakupendi!
Mapenzi ni nguzo ya maisha yetu, kama ukifanikiwa kumpata mpenzi ambaye atakupenda na wewe ukampenda ni wazi kuwa maisha yako yatakuwa yenye furaha na hakika utafurahia maisha yako na huyo mwandani wako. Mapenzi yapo hivyo na kama ukijaribu kuyabadilisha utaumia mwenyewe!
Wakati mwingine unaweza ukapendwa na mpenzi ambaye hujampenda, unadhani kuna ulazima wa wewe kulazimisha kumpenda? Moyo wako umeshazungumza na wewe, umekuweka wazi kuwa hauna mapenzi ya dhati kwa mtu huyo, kwa nini ujilazimishe? Tatizo hili mara nyingi huwa kwa wanawake zaidi!
Anatokea mwanaume anampenda sana, anapomtongoza anajikuta kuwa hampendi, anachokifanya ni kumwambia kuwa atamjibu baadaye! Lengo la kumwambia hivyo ni kwa ajili ya kujipanga na kufikiria! Mapenzi hayafikiriwi ndugu zangu!
Kama mtu unampenda, unapomuona tu siku ya kwanza, moyo wako hutetemeka juu yake na hutamani uambiwe kitu fulani na huyo aliyeuteka moyo wako ghafla. Hii inamaana kuwa atakapokuambia kuwa anakupenda, huwezi kusubiri zaidi, hutakuwa na kitu cha kusubiri, ni nafasi uliyokuwa ukiisubiria kwa hamu sana, na lazima utamkaribisha!

‘KUJITAHIDI KUPENDA!’
Baadhi ya wasichana, akitongozwa na mwanaume ambaye anaona wazi kuwa hampendi, lakini akawa na mali au uwezo mkubwa kifedha, huamua kumkubali kwa lengo la kupata vitu vya mwanaume huyo. Hufanya hivyo ajidanganya kuwa ‘atajitahidi’ kumpenda taratibu akiwa naye ndani ya uhusiano.
“Pesa anazo, magari anayo, hata kama simpendi nitajitahidi kumpenda taratibu,” ni kauli ya kawaida sana kwa wasichana ninaowazungumzia hapa.
Baada ya wazo hili kuingia akilini, huwa hana muda wa kusubiri zaidi, anakubali na wakati mwingine huweza kuingia hata katika ndoa.

NI HATARI KUBWA!
Kuna mengi ambayo yanaweza kutokea kwa kujidanganya kuingia kwenye sehemu ambayo huna mapenzi nayo. Kubwa zaidi ni ile hali ya kutokutosheka na mwenzi uliyenaye.
Anaweza akakupa kila kitu lakini ukakosa penzi la dhati, ambalo ndio msingi wa maisha. Unajua kama kuna mtu anakupenda na wewe unampenda, unajihisi furaha na amani siku zote.
Madhara makubwa zaidi ni pale utakapojikuta ukiingia katika uhusiano na mwanaume mwingine kwa ajili ya kusaka penzi la dhati! Unajua kitakachotokea? Kama si kuambulia kipigo, basi utafukuzwa nyumbani kwa mwanaume huyo. Yote hayo ya nini?

BAKI NA HILI
Kamwe usijaribu kuingia katika mkumbo huu, mkumbo wa kuingia kwenye uhusiano ukiwa na uhakika huna mapenzi ya dhati. Ni jambo gumu ambalo huweza likaharibu maisha yako kabisa.
Tambua thamani ya mapenzi kwa kuheshimu hisia zako za ndani. Unapoamua chochote kuhusu mapenzi ujue unaamua jambo linahusu maisha yako.

No comments:
Post a Comment