Sweden yaondoka kwa kishindo

Wafaransa itawabidi kucheza kwa hima zaidi watakapokutana na Uhispania
Bao lililoingia wavuni kwa
ustadi kutoka kwa Zlatan Ibrahimovic limeisaidia Sweden kuishinda
Ufaransa magoli 2-0 katika mechi ya kundi D usiku wa Jumanne, na
kuhakikisha wameisukuma Ufaransa katika nafasi ya pili katika kundi, na
pia kuilazimisha kukutana na mabingwa watetezi Uhispania katika mechi ya
robo fainali ya Euro 2012.
Ufaransa walilemewa katika mechi hiyo, na Ola
Toivonen alikaribia kuiletea Sweden bao la kwanza alipogonga sehemu ya
nje ya mwamba wa goli.
Hatimaye Ibrahimovic alipata bao kupitia mkwaju kutoka yadi 15, baada ya kusukumiwa mpira kutoka kwa Sebastian Larsson.
Olivier Giroud alifunga kwa kichwa na kuiwezesha Sweden kupata bao lao la pili.
Kushindwa kwa Ufaransa kuna maanisha hatua yao
ya kucheza pasipo kushindwa katika msururu wa mechi 23 zilizopita tangu
waliposhindwa wakiwa nyumbani na Belarus mwezi Septemba mwaka 2010
imesitishwa.
Huo ndio muda mrefu zaidi ulioandikishwa timu kucheza pasipo kushindwa kwa upande wa mechi za kimataifa.
Ufaransa wameshindwa baada ya mechi 24 za
kimataifa, na kocha Laurent Blant sio tu atakuwa na wasiwasi katika
kupambana na mabingwa wa Ulaya na wa dunia pia, bali pia kuhusiana na
timu yake kucheza mchezo wa kiwango duni.
Sweden tayari walikuwa wameondolewa katika
mashindano baada ya kushindwa katika mechi zao mbili za mwanzo, lakini
nia yao ilikuwa ni kucheza kadri ya uwezo wao kabla ya kurudi nyumbani.
Jumapili iliyopita, wachezaji hao walikataa
ushauri wa meneja Erik Hamren wa kupumzika, na badala yake waliamua
kuitumia siku hiyo katika kufanya mazoezi zaidi.
No comments:
Post a Comment