Thursday, June 28, 2012

RAY AZINDUA FILAMU YA SOBING SOUND KWA KUTOA MSAADA AKISHIRIKIANA NA STEPS...!!!

 Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre  kilichopo Kinondoni, Bi. Zainabu Bakari. Vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage.
 Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre  kilichopo Kinondoni, Bi. Zainabu Bakari. Vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage.
Msanii wa Filamu Nchini Vicent Kigosi 'Ray' katikati na Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps Ignatus Kambarage wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Ray kugawa vyakula mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre vilivyotolewa na Kampuni ya Steps wakati wa Uzinduzi wa filamu yao Mpya ya Sobing Sound.
---
MSANII wa filamu nchini  Vicent Kigosi 'Ray'  amezindua filam yake  mpya inayojulikana kama 'SOBING SOUND'.

Filamu hiyo imezinduliwa kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua Ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filamu hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 1.5  kwa niaba ya Kempuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam

Akizungumza mara baada ya kuzindua filamu hiyo akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba  watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha huku wengine wakiendelea kutaabika kitendo ambacho si kizuri.

Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zake zote zinafanya vizuri na atahakikisha japo anatoa kidogo kwa namna yoyote ile kwa kuwakumbuka watoto yatima kwa kila filamu anayotoa.

Alisema msaada uliotolewa kwa watoto yatima hautaishia kwao bali ataendelea kutoa kile atakachokipata kupitia filamu hiyo kuwasaidia na wale wasiojiweza amesema kampuni ya  Steps Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa wasanii kutambulika na kutushawishi tuwe tunawakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu.


Nae mmoja wa wakilishi wa Kampuni ya Steps Ignatus Kambarage amesema swala la watoto yatima ni letu sote na wala halichagui kwa kuwa tunawajibu na angalau kidogo tunachokipata kupitia filamu zetu tunarudisha kwa kutoa shukrani zetu.
-- 
Rajabu Mhamila Super D

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...