BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Monday, June 18, 2012


MWANAFUNZI WA SAINT AUGUSTINE APOTEA KIMAZINGARA BAADA YA KUONANA NA MWANAUME WALIYEKUTANA FACEBOOK HOTELINI

Angalieni sana hii kitu inaitwa Facebook aisee,wote wadada na wakaka,kuna vitu vya ajabu sana vinaendelea humu...Kuna wadada wanajiuza wako humu ni wewe tu na muda wako unapewa huduma unalipia...Kuna wachawi humuhumu...Kuna freemasons humu wakikutumia Friend request uki-accept tu uko hatarini kufa...Kuna mengi sana sana!

Kwa leo kuna hili tukio linaloripotiwa kutokea Mwanza,siku chache tu nyuma...

Kuna Mwanafunzi wa kike,mrembo kweli wa chuo almaarufu pale Mwanza kinaitwa Mtakatifu Augustino....Amekutana na Mwanaume Facebook,wakatokeana Fresh tu,ila jamaa dizaini yuko Kenya..

Baada ya muda flani wa kuwasiliana wakakubaliana wawe wapenzi na kuahidiana kuonana soon...

Mwanaume akatimiza ahadi wiki chache zilizopita,akakwea pipa akaja Mwanza kumuona mchumba wa burebure aliyempata kupitia kwa hisani ya Mark Zuckerberg,owner wa mtandao huu wa Facebook..

Wamekula bata,imefika usiku wakakubaliana waende zao hotelini kula tunda bana...Kufika kule wameingia room...

UTAMU KOLEA
Walipochojoa mambo flani yanaitwa nguo yule msichana akagundua jamaa hayuko fresh kwenye sehemu za 'kinyume cha wazi',dizaini kama jamaa ameoza flani bwana...Demu akaona ah ah,hapa mechi haitachezeka bana...

Mshkaji akachomoa silaha na kutishia kumshoot kama ataondoka....Mungu jalia purukushani za hapa na pale yule msichana akafanikiwa kuchoropoka mikononi mwa mchizi...Akakimbia kwenda chuo..

Kufika chuo akawasimulia rafiki zake yaliyojiri huko hotelini.....

Ile kumaliza tu kuwasimulia...BALAA! Yule msichana hali yake ikabadilika akaanza kuoza bana,sehemu za 'kinyume cha wazi' kama jamaa...

Ikabidi wenzie wamkodishie Taxi kuwahi hospitali...ila sasa Cha ajabu...Kabla hawajafika mbali yule msichana akatoweka kwenye Mazingira ya kutatanisha...Yaani akayeyuka kabla hawajafika hospitali...

Mpaka habari hii inafika mikononi mwa ripota wa Blogu hii,huyo Msichana hajulikani alipo!

Inatisha...Dizaini jamaa ni mchawi au anatumia nguvu za kichawi na mwanafunzi ndio huyo amepotea na haijulikani nini kimetokea...

BE VERY CAREFUL....Haikatazwi kudate Facebook ila Just be Careful,you never know how dangerous the person you are messing with is....

Mi mwenyewe nimesisimka,ila imebidi nishee na wewe.....STAY SAFE!

2 comments:

  1. HABARI ZILIZOTUFIKIA NI KUWA HUYO DEMU WA ST AUGUSTINE AMEPATIKANA LAKINI KAWA ZEZETA IMEBIDI WAZAZI WAKE WAITWE WAMEKWENDA MWANZA KUMCHUKUA MTOTO WAO SASA SIJUI ITAKUWAJE ATAPONA ARUDIE HALI YAKE??? AU NDO AMESHAHARIBIKAA?? EE MWENYEZI MUNGU MSAIDIE BINTI HUYO. JAMANIII CHONDE CHONDE NA USO WA KITABU UTATUMALIZA............... HV A GUD DAY

    ReplyDelete
  2. thnx sana kwa kutujuza huyo atakuwa kafumbwa mdomo asiseme aliyoyaona facebook balaa tuwe makini

    ReplyDelete

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...